February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

StarTimes yasalimu amri, yaomba radhi wateja wake

Spread the love

KAMPUNI ya Star Media (T) Ltd inayomiliki king’amuzi cha StarTimes imesalimu amri kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA). Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku moja baada ya TCRA kueleza dhamira ya kuifungia kampuni kwa kupuuza kufuata sheria zinazosimamia mawasiliano na urushaji wa vipindi kupitia king’amuzi hicho.

StarTimes imewaomba radhi wateja wake pendwa na umma kwa ujumla kwa kutopata chaneli za bure kwa muda sasa.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji Star Media(T)Wang Xiaobo amesema leo kuwa hiyo imesababishwa na kukosekana kwa elimu na mawasiliano mazuri kuhusu aina ya tofauti za dikoda (ving’amuzi) tulizonazo, ambayo yamesababisha kwa wateja wao kuendelea kulipia chaneli za bure.

“Tunapenda kuwafahamisha wateja wetu kuwa ziko aina mbili za dikoda, ya kwanza ni ile ya Chaneli za bure (FTA) ambayo mteja halazimiki kila mwezi ili kutazama chaneli za bure.

“Na nyingine ni ya chaneli za kulipia, ambayo mteja atatakiwa kulipia kifurushi chake kila mwezi,” amesema

Ameongeza kwa wateja wapya, dikoda (ving’amuzi) hizo zinapatikana kwenye maduka yao pamoja na mawakala wao, lakini kwa wateja ambao tayari wameshanunua dikoda (ving’amuzi) za kulipia wanaweza kubadilisha dikoda (ving’amuzi) zao kuwa FTA kwa kutembelea katika ofisi zetu na kupata utaratibu.
Amesisitiza Star Media (T) Ltd, itaendelea kuzingatia masharti yote ya leseni, pia inaufahamisha umma kwamba imekubali kufuata na kutekeleza maagizo ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ikiwamo kulipa faini ambayo tayari imeshaanza.

Pia wanawafahamisha umma wa watanzania kwamba sasa wanaweza kuendelea kufurahia chaneli za bure na huduma zetu kwa ujumla.

error: Content is protected !!