January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Stars yakaa kileleni kundi J

Spread the love

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imerejea tena kwenye usukani wa kundi J, katika harakati za kutafuta tiketi za kufuvu fainali za kombe la Dunia zitakazofanyika Qatar 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Mabadiliko hayo yamekuja mara baada hii leo tarehe 10 Oktoba 2021, kupigwa michezo miwili kwenye kundi hilo kwa mzunguko wa pili.

Katika mchezo wa kwanza uliofanya Stars kufufua matumaini, walifanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 1-0, wakiwa ugenini dhidi ya Benin.

Bao hilo pekee la Tanzania kwenye mchezo huo, lilifungwa na mshambuliaji Simon Msuva kwa shuti kali kwenye dakika ya 6.

Matokeo hayo yaliwafanya Stars, kufikisha pointi saba, sawa na Benin lakini kukiwa na utofauti wa mabao yakufungwa na kushinda.

Mchezo wa pili uliofuta uliwakutanisha Madagascar ambao walikuwa nyumbani dhidi ya Jamhuri ya Congo, na wenyeji hao kufanikiwa kuondoka na ushindi wa bao 1-0.

Kipigo hiko kiliwafanya Congo kusalia na pointi zaao 5, kwenye nafasi ya tatu, huku Madagascar akiendelea kuburuza mkia akiwa na alama tatu, ukiwa ndio mchezo wao wa kwanza kushinda.

Kundi hilo sasa limebakisha michezo miwili kwa kila timu, ambayo itapigwa tarehe 11 na 14, Novemba 2021, ambapo Stars itaanza kushika Dimbani nyumbani dhidi ya Jamhuri ya Congo, na baadae wataenda ugenini kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Madagascar.

error: Content is protected !!