Monday , 26 February 2024
Home Kitengo Michezo Stars yaingia kambini kuwawinda Cape Verde
Michezo

Stars yaingia kambini kuwawinda Cape Verde

Emmanuel Amunike, Kocha wa Taifa Stars
Spread the love

TIMU ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars imeingia rasmi kambini leo kujiwinda na mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu kwa michuano ya mataifa hutu ya Afrika dhidi ya Cape Verde unaotarajiwa kuchezwa 12 Octoba, 2018 ugenini kwenye mji wa Praia. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Mazoezi ya timu hiyo yataanza kesho kwenye Uwanja vya JKM Park uliopo Mnazi Mmoja chini ya kocha mkuu Emmanuel Amunike baada ya ligi kuu kusimama.

Stars ambayo inashika nasafi ya tatu kwenye kundi L baada ya kucheza michezo miwili na kufanikiwa kujipatia alama mbili, huku kundi hilo likiongozwa na timu ya Taifa ya Uganda wenye alama nne, wakifuatiwa na Lesotho wenye alama mbili na huku Cape Verde akiwa wa mwisho baada ya kupata alama moja.

Wachezaji ambao wataingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo ni Aishi Manula (Simba), Salum Kimenya (Tz Prisons), Frank Domayo(Azam FC), Salum Kihimbwa (Mtibwa), Kelvin Sabato (Mtibwa), David Mwantika (Azam FC),  Ally Abdulkarim Mtoni (Lipuli),  Mohamed Abdulrahiman (JKT Tanzania).

Wengine ni Beno Kakolanya (Young Africans), Hassan Kessy (Nkana,Zambia), Gadiel Michael (Young Africans), Abdi Banda (Baroka, Afrika Kusini), Aggrey Morris (Azam FC), Andrew Vicent (Yanga), Himid Mao (Petrojet, Misri), Mudathir Yahya (Azam FC),

Pia wamo Simon Msuva (Al Jadida, Morocco), Rashid Mandawa (BDF, Botswana), Farid Mussa (Tenerife, Hispania), Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (Al Hilal, Sudan), Shabani Chilunda (Tenerife, Hispania), Yahya Zaydi (Azam FC), Kelvin Yondan (Yanga), Paul Ngalema (Lipuli), Jonas Mkude (Simba), John Boko (Simba), Shomari Kapombe (Simba), Feisal Salum (Yanga) na Abdallah Kheri (Azam FC).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Wizara yaahidi kuboresha, kuimarisha michezo

Spread the loveIkiwa ni saa kadhaa baada ya kumalizika kwa mashindano ya...

Habari MchanganyikoMichezo

Nje jogging yanyakua medali 20 Kili Marathon

Spread the loveTimu ya riadha ya Wizara ya Mambo ya Nje na...

Michezo

Siku ya kukusanya maokoto ni leo, usipange kukosa

Spread the love  HATIMAYE Jumamosi imefika ndugu mteja wa Meridianbet na mechi...

Michezo

Kuwa milionea na Meridianbet ni rahisi sana

Spread the love  JE, unajua kuwa leo hii ni siku nzuri kwako...

error: Content is protected !!