August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Stars yaibuka mbabe mbele ya Somalia

Spread the love

 

TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Somal;ia katika kutafuta tiketi ya kufuzu kwa fainali za mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo ambao Stars ilikuwa ugenini licha ya kupigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, kufuatia Somalia kuchagua Uwanbja huo kuchezea mchezo wao wa nyumbani.

Bao la Stars kwenye mchezo huo liliwekwa kambani na Abdul Suleiman Sopu kwenye dakika ya 63, na kuitanguliza Stars mguu moja mbele kuvuka kwa hatua inayofuata.

Ushindi huo unaumhimu mkubwa kwa Taifa Stars kuelekea mechi ya marudiano itajayochezwa kwenye uwanja huo huo, Tarehe 30 Julai 2022.

Kwenye mchezo huo wa marudiano Stars anahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili waweze kufuzu kwa hatua inayofuata ya mzunguko wa pili ambapo watamenyana dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda.

Stars ambayo iliingia dimbani hii leo chini ya kocha Kim Poulsen ilionesha mchezo mzuri katika dakika zote 90 za mchezo, kwa kulisakama lango la wapinzania wao muda wote.

Pamoja na kucheza muda wote langoni mwa wapinzani wao, Stars ilipata pigo kwenye dakika za mwishoni kufuatia kuumia kwa mlinda mlango wake Aishi Manula, na nafasi hiyo kuchukuliwa na mlinda mlango namba mbili Abutwalibu Mshery.

error: Content is protected !!