TIMU ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inashuka dimbani kucheza na Namibia kwenye michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Mchezo huo wa pili kwa Taifa Stars, utachezwa Uwanja wa Limbe/Buea nchini Cameroon kunakofanyika mashindano hayo leo Jumamosi saa 4:00 usiku.
Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imesema, wachezaji watatu wa kikosi hicho kinachonolewa na Mburundi, Etienne Ndayiragijje ambao ni; John Bocco, Erasto Nyoni na Ibrahim Ame ambao wako chini ya uangalizi wa madaktari.

Wachezaji hao ambao wote kwa pamoja wanaitumikia Klabu ya Simba ya Dar es Salaam, waliukosa mchezo wa kwanza dhidi ya Zambia ambapo Stars ililala kwa magoli 2-0.
Stars iko kundi D pamoja na Zambia, Namibia na Guinea ambayo inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi tatu sawa na Zambia ambazo zote zilishinda michezo yao ya kwanza.
Mchezo wa leo Jumamosi, kati ya Stars na Namibia, zinakutana zikiwa na kumbukumbu ya kupoteza michezo yao ya kwanza.
Leave a comment