Tuesday , 5 December 2023
Home Kitengo Michezo Stars kuingia kambini kesho
Michezo

Stars kuingia kambini kesho

Spread the love

KIKOSI cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kesho tarehe 5 Mei, 2021 kinatarajia kuingia kambini kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Timu ya Taifa ya Malawi katika kujiweka sawa kuelekea mchezo wa kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia litakalofanyika Qatar mwakani. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Kikosi kitakachoingia kambini kesho kitakuwa na wachezaji 27 mara baada ya kuitwa na kocha mkuu wa timu hiyo Kim Pulsen wiki moja iliyopita.

Wakati timu hiyo ikingia kambini Ligi Kuu Tanzania Bara itakwenda kusimama kwa wiki mbili mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa jana kati ya Simba dhidi ya Ruvu Shooting uliopigwa kwenye Uwanja wa Ccm Kirumba, Mwanza.

Kambi hiyo watakayoingia kesho itakuwa ya awamu ya kwanza huku awamu nyingine ikiwa mwezi Agosti m,ara baada ya kukamilika kwa Ligi Kuu Tanzania Bara na Poulsen alisema kuwa haitakuwa na mabadiliko makubwa.

“Kambi ya kwanza itakuwa mwezi Juni ambapo tutakaa kwa wiki mbili na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi ambao wamefuzu kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) na kambi nyingine itakuwa mwezi Agosti ambapo Ligi Kuu itakuwa imesha, ” alisema kocha huyo.

Kim Poulsen Kocha wa Taifa Stars

Kocha huyo alitoa sababu kwanini kikosi hiko kinaingia kambini mapema ni kutaka timu hiyo ipate muda mrefu wa kujiandaa kutokana na idadi kubwa ya wachezaji aliyowaita wanacheza kwenye Ligi ya ndani na kutoa pendekezo hilo kwa TFF.

“Kama tukiendelea kufanya vilevile tutaendelea kupata matokeo yale yale haya ndio niliwaambia TFF kwa hiyo tunatakiwa kubadilika, najua asilimia kubwa ya wachezaji niliowaita wanacheza kwenye ligi ya ndani, ” alisema Poulsen.

Wachezaji watakaoikingia kambini kesho ni walinda mlango Juma Kaseja (Kmc), Aishi Manula (Simba) na Metacha Mnata (Yanga) huku wengine Shomari Kapombe (Simba SC), Israel Mwenda (KMC FC), Mohammed Hussein (Simba SC), Edward Manyama (Ruvu Shooting), Erasto Nyoni (Simba SC), Bakari Mwamnyeto (Yanga SC), Kennedy Juma (Simba SC), Dickson Job (Yanga SC), Nickson Kibabage (Youssoufia fc – Morocco).

Upande wa viungo wapo Simon Msuva (Wydad AC – Morocco), Mudathir Yahya (Azam FC), Mzamiru Yassin (Simba SC), Feisal Salum (Yanga SC), Salum Abubakar (Azam FC), Braison Nkulula (Azam FC), Iddy Suleiman Nado (Azam FC), Mbwana Samatta (Fenerbahce FC – Uturuki), John Bocco (Simba SC), Abdul Hamis Suleiman (Coastal Union), Ayoub Lyanga (Azam FC), Denis Kibu (Mbeya City), Meshack Abraham (Gwambina FC), Novatus Dismas (Maccabi Tel Aviv – Israel)na Yusuf Mhilu (Kagera Sugar).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaMichezo

Mwana FA anogesha Tamasha la Exim Bima Festival

Spread the loveNAIBU Waziri Wa Utamaduni, Sanaa Na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana...

Michezo

Manchester City dhidi ya Tottenham ni usiku wa kisasi

Spread the love KIPUTE kati ya klabu ya Manchester City dhidi yaTottenham Hotspurs...

Michezo

Wikiendi ya kutamba na Meridianbet hii hapa usikubali kuikosa

Spread the loveMERIDIANBET wanakwenda kukupa nafasi ya kutambawikiendi hii kupitia ODDS KUBWA walizoweka...

Michezo

Fernandes hakamatiki Man Utd, mahesabu ni kuifunga Bayern

Spread the love  NAHODHA wa Manchester United, Bruno Fernandes, alikuwa na kiwango...

error: Content is protected !!