May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Stars kuingia kambi leo, wachezaji Simba, Yanga warejea

Spread the love

 

TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inaingia kambini hii leo Agosti 24, 2021 kujiandaa na michezo miwili ya kufuzu fainali za kombe la Dunia zikazofanyika nchini Qatar, mwakani huku wachezaji kutoka klabu za Simba na Yanga wanatarajia kujinga na kambi hiyo muda wowote. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Kikosi hiko cha wachezaji 28, kitaingia kambini chini ya kocha Kim Poulsen kwa ajili ya kujianda na michezo hiyo miwili ya kundi J.

Katika idadi hiyo ya wachezaji iliyoitwa, klabu za Simba na Yanga zimetoa jumlya ya wachjezaji 13, ambao tayari wameshaanza safari kutoka nchini Morocco siku ya jana ambapo timu hizo zote mbili zilikita kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindao 2021/22.

Kambi hiyo itakuwa ya siku tano, kabla ya kuanza safari kuelekea Jamhuri ya Kidokrasia ya Congo, kwenye mchezo wao wa kwanza utakaopigwa Septemba 2, mwaka huu kwenye dimba la TP Mazembe lililopo Lubumbashi.

Kim Poulsen

Mara baada ya mchezo huo Stars itarejea nyumbani, kwenye mchezo wake wa pili dhidi ya Madagascar utakaopigwa Septemba 7, 2021 kwenye Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, majira ya saa 10 jioni.

Wakati alipoita kikosi hiko mbele ya waandishi wa Habari Agosti 19, mwaka huu kwenye makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Poulsen alisema kuwa kwa sasa ameita jumla ya wachezaji 28, watakaoingia kambini, lakini wachezaji watakaosafiri watakuwa ni 23.

“Kwa sasa nimeita wachezaji 28 watakaoingia kambini, ila watakaosafiri ni wachezaji 23, nataka niende na idadi kubwa ili ikitokea changamoto yoyote kwa mchezaji basi tuwe na mbadala hasa kwenye upimaji wa virusi vya corona.” Alinena Poulsen

Wachezaji 28, ambao wameitwa kwenye kikosi hiko ni Aishi Manula,  Shomari Kapombe, Israel Mwenda, Erasto Nyoni, Mohamed Hussein, Kennedy Juma, John Bocco na Mzamiru Yassin wote kutoka Simba.

Wengine ni Ramadhani Kabwili, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Zawadi Mauya na Feisal Salum wote kutoka klabu ya Yanga.

Kutoka klabu ya Azam FC Wilbol Maseke, Lusajo Mwaikenda, Abdulrazack Mohamed, Edward Manyama, Ayoub Lyanga, Mudathir Yahya, Salum Abubakar na Iddy Selemani.

Wengine ni Metacha MnataNickson Kibabage [Youssoufla FC-Morocco], Meshack Mwamita (Gwambina FC), Novat Dismas (Maccabi Tel Aviv-Israel), Abdul Hamis Seleman (Coastal Union), Mbwana Samatta (Fenerbahce-Uturuki) na Simon Msuva (Wydad Athletic-Morocco).

error: Content is protected !!