November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Stars basi tena, yatupwa nje kufuzu kombe la Dunia

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kikiwa mazoezini

Spread the love

 

TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imetupwa nje rasmi kwenye kinyang’anyiro cha kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia mara baada ya Benin kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Madagascar. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Stars ambayo leo imepoteza mchezo dhidi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, kwa mabao 3-0, kwenye dimba la Benjamin Mkapa, matokeo ambayo yamewafanya kuaga rasmi kwenye harakati za kufuzu kombe la Dunia, litakalofanyika 2022, nchini Qatar.

Mara baada ya Benin kupata ushindi dhidi ya Madagascar, imefikisha jumla ya ponti 10, huku ikibakiwa na mchezo mmoja mkononi ambao ni dhidi ya Congo wenyejumla ya pointi 8.

Kama Stars ikishinda mchezo wake wa mwisho dhidi ya Madagascar itafikisha pointi 10, sawa na Benin ambaye anayeitaji sare au ushindi wowote ili aweze kufuzu kwa hatua inayofuata.

Mchezo huo wa mwisho kati ya Benin na Congo utacheza, tarehe 14 Novemba 2021, jijini Lubumbashi, ambapo kama Congo watashinda watafikisha pointi 11, na kuweza kufanikisha kufuzu kwa hatua inayofuata.

Kwa matokeo yoyote yatakayo patikana kwenye mchezo huo kati ya Benin dhidi ya Congo yatainyima fursa Stars kufuzu kjwa hatua inayofuata, hata ikipata ushindi dhidi ya Madagascar.

Nafasi pekee ya kujitengenezea mazingira mazuri ilikuwa ni kupata matokeo kwenye mchezo wa leo, nakushindwa kufanya hivyo na kukubali kichapo cha mabao 3-0.

Bao la kwanza la Coongo kwenye mchezo huo lilipatikana kwenye dakika ya sita liliwekwa kambani na Kakuta mara baada ya mlinzi wa kati wa Taifa Stars Dikson Job kufanya makosa kwa kupoteza pasi, na kufanya mpira huo kwenda mapumziko Stars ikiwa nyuma kwa bao moja.

Dakika ya 66, Iduma Fasika beki wa kati wa Congo alipachika bao la pili, na dakika 19 baadae Malango aliweka kambani bao la tatu kwenye dakika ya 85 na kufanya mchezo kutamatika kwa jumla ya mabao matatu kwa bila.

error: Content is protected !!