Friday , 9 June 2023
Home Habari Mchanganyiko STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML
Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the love

SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika shughuli za uchorongaji miamba ya madini baada ya kusaini mkataba wa thamani ya Sh bilioni 55.2 na Kampuni ya Geita Gold Mine Limited (GGML). Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

GGML imeiongezea STAMICO kandarasi hiyo ya miaka miwili kwa lengo la kuendelea kuchoronga miamba ndani ya mgodi huo uliopo mkoani Geita baada ya kufanya vizuri katika kandarasi ya awali ya miaka mitatu.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Elder Damon (kushoto) akisaini mkataba kati ya kampuni hiyo na Shirika la Madini la Taifa Stamico) wenye thamani ya Sh bilioni 55.2 kwa lengo la kuendeleza shughuli za uchorongaji miamba kwenye migodi ya kampuni hiyo. Kulia na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dk. Venance Mwasse.

Makubaliano hayo yamesainiwa tarehe 27 Machi mwaka huu mkoani Geita mbele ya Waziri ya Madini, Dk. Doto Biteko pamoja viongozi wengine wa wizara hiyo na GGML.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dk. Biteko ameipogeza STAMICO kwa hatua ya kupata kandarasi kubwa na kusisitiza kufanya kazi hiyo kwa weledi na uaminifu kwa kipindi chote cha mkataba ili kuvutia kampuni nyingine.

Pia ameiongeza GGML kwa kuwa mstari  wa mbele katika kuzingatia matakwa ya sheria ya madini kuwapa watanzania kandarasi mbalimbali za mgodi huo ‘local content’.

“Nimefurahi kuona Kampuni za wazawa wakipata kandarasi kama hizi hapa nchini tofauti na kipindi cha nyuma waliokuwa wanapata kandarasi ni makampuni ya kigeni” alisema Dk. Biteko.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dk. Venance Mwasse amesema mkataba huu ni udhibitisho kuwa watanzania wanaweza kushiriki kikamilifu katika kandarasi zinatokea katika mnyororo wa thamani wa madini.

Ametaja mafanikio makubwa ya mkataba huo ni pamoja na ongezeko la mapato kwa Shirika na kuongeza ajira kwa Watanzania.

“Tunajivunia kufanya kazi na GGM kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitatu kwa mfululizo na kwa kipindi chote tumekuwa na ushirikiano mzuri.

“Mgodi wa GGM umekuwa mfano wa kuigwa katika kuthamini na kuamini Kampuni za Kitanzania kufanya kazi za uchorongaji (local content) hivyo kumesababisha kupata tena kandarasi nyingine kubwa kama hii”

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Elder Damon alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa kanuni za ushirikishaji wazawa kwenye shughuli za uchimbaji madini mwaka 2018, idadi ya wafanyabiashara watanzania waliofanikiwa kushinda kandarasi mbalimbali ndani ya mgodi huo, imeongezeka.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Elder Damon akizungumza katika hafla hiyo.

“Nia yetu imekuwa kusaidia jamii kwa kuwapa ujuzi ili kuwawezesha kushindana kikamilifu. STAMICO imekuwa ikitoa huduma za uchorongaji miamba ndani ya GGML, kusaidia programu za uchimbaji wa wazi tangu Septemba 2020.

“STAMICO imetoa huduma za uchorongaji miamba kwa viwango vya juu kwa kuzingatia usalama na ufanisi katika sekta ya uchimbaji madini kulingana na malengo ya sekta hii. Makubaliano haya na STAMICO yanaonyesha uungaji mkono unaoendelea katika ukuzaji wa ujuzi na utaalamu kuhusu uchorongaji miamba na utafiti wa madini nchini,” alisema Damon.

Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya STAMICO, Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo amesema STAMICO haitosita kuwachukulia hatua wale wote ambao wataonesha dalili za makusudi za kurudisha nyuma jitihada  au kukwamisha matokeo chanya kwa Shirika.

1 Comment

  • Wapambania haki za Binadamu wamebuni Mbinu za Mwanamke kupata SIFA ZINAZOSTAHIZI KWA KUMWEKEA VIKWAZON VYA KILA MTU ANATAKIWA KUMUONA MWANAE ALIYEMZAA (MZEE/kabila ANATAKA URAISI KULE ULIKOENDA KUONA)…

    KAMA UNA MATOTO WA KIKE UNAJUA FURSA ULIONAYO KAMA MZAZI

    KAMA UNA MTOTO WA KIUME UNAJUA FURSA ULIYONAYO USIMSAHAU BASH YUPO KULE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi zaidi ya 100 wapigwa msasa wa udereva kukabiliana na ajali

Spread the love  KATIKA kuhakikisha wimbi la ajali za barabarani zinapungua kama...

Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali yakana kuhamisha kwa nguvu jamii ya Kimasai Loliondo

Spread the loveWAZIRI wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro,...

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

error: Content is protected !!