Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko STAMICO wachimbaji wadogo wanakopesheka
Habari Mchanganyiko

STAMICO wachimbaji wadogo wanakopesheka

Spread the love

SERIKALI imesema kuwa tayari imeongea na baadhi ya Taasisi za kifedha nchini  na kufikia makubaliano  juu ya kutoa mikopo kwa wachimbaji wadogo hali ambayo itawatoa katika wimbi la umasikini katika siku za baadaye.

Pia imesema itaendelea kutoa elimu ya kutosha kwa kundi la wachimbaji wadogo wenye usikivu hafifu ambao wanachimba madini ya dhahabu katika eneo la Nyakafuru katika Mkoa wa kimadini wa Mbogwe. Anaripoti Paul Kayanda, Mbogwe   (endelea).

Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dk. Venance Mwasse (wa kwanza kushoto) akishuhudia zoezi la ugawaji wa vifaa hivyo vilivyogharimu zaidi ya Sh milioni sita.

Hayo yalisemwa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Dk. Venance Mwasse katika hafla ya ugawaji wa vifaa kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu kutoka katika kikundi cha wachimbaji wa madini hayo wenye usikivu hafifu wilayani Mbogwe.

Zoezi hilo la ugawaji wa vifaa kwa wachimbaji hao linaendela sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya STAMICO tangu kuanzishwa kwake mwaka 1972.

Mwasse alisema tayari wameshafanya mazungumzo na baadhi ya taasisi za kifedha ikiwemo Benki za CRDB, NMB pamoja na KCB na kufikia makubaliano na kuongeza kuwa shirika hilo ndio litakuwa mdhamini kwa wachimbaji hao.

Alisema kama mabenki yakitaka taarifa juu ya wachimbaji hao itabidi kuwasiliana na STAMICO na kuongeza ili kupata mikopo hiyo tayari wameshaanza kutoa elimu kwa kundi hilo lenye usikivu hafifu.

Aliwataka wachimbaji hao kwa sasa kuanza utaratibu wa kurasimisha maeneo yao ya uchimbaji na kuongeza kuwa lazima watumie fursa hiyo ili kukopesheka na taasisi hizo na hivyo kujikomboa katika wimbi la umasikini kwa makundi hayo.

Aidha, aliendelea kusima kuwa shirika hilo litaendelea kuwashika mkono wachimbaji hao wenye usikivu hafifu kwa kuwa vifaa va kuwakinga na madhara wakati wote wakiwa katika shughuli zao za kiuchimbaji.

Kwa upande wake Meneja wa CRDB Tawi la Mbogwe, Simoni Mapesa alisema tayari wameingia makubaliano na STAMICO kuiona jinsi ya kuwasaidia kundi hilo la wachimbaji wenye usikivu hafifu na kuongeza kuwa wapo tayari kufanya kazi hiyo kwa sasa.

Alisema wapo tayari kufanya kazi na taasisi hizo ambazo zipo katika maeneo ya madini na kuongeza kuwa benki hiyo ipo katika hatua ya kuwawezesha watendaji wake kupata elimu kwa ajili ya kywahudumiaa wachimbaji wadogo.

‘Sekta hii inahitaji taarifa za uhakika na za kutosha kutoka kwa wataalamu ili kujua sehemu gani yenye mali na mwisho wa mwezi huu tutafikia matawi ya benki katika maeneo yote yenye madini,” alisema.

Aliongeza kuwa matawi yaliyopo katika maeneo yenye madini ndio yatakayofikiwa na kuongeza kuwa wanahitaji kuwapa elimu watendaji  kwa lengo la kujua nini  kinahitajika kwa wachimbaji wadogo waliopo katika maeneo hayo ya uchimbaji wa madini.

Naye mgeni rasmi katika makabidhiano hayo Katibu tawala Wilaya ya Mbogwe, Christopher Bahari alisema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akiwapigania wachimbaji wadogo hasa walemavu  na kuongeza kuwa hata katika halmashauri zetu kuna fungu kwa ajili ya kuwasaidia kundi hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!