November 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Staa wa movi aua mwanamke kwa bunduki wakati wa kutengeneza filamu

Alec Baldwin

Spread the love

 

MWANAMKE  mmoja amefariki dunia huku mwanaume mmoja akijeruhiwa baada ya muigizaji Alec Baldwin kufyatua risasi kwa kutumia bunduki ya maigizo wakati wakiandaa filamu yao huko New Mexico nchini Marekani. Anaripoti Mwandishi wetu… (endelea).

Polisi katika jimbo hilo la Marekani wamesema Baldwin alitoa silaha hiyo wakati wa utengezaji wa filamu yake.

Mwanamke huyo alipelekwa hospitalini lakini alifariki kutokana na majeraha aliyopata.

Hata hivyo, mwanaume aliyejeruhiwa – ambaye ni mkurugenzi wa filamu, alikuwa akipokea huduma ya dharura.

Msemaji wa Baldwin aliliambia shirika la habari la AP kwamba kisa hicho kilihusisha utumiaji mbaya wa bunduki ya maigizo.

Mwanamke huyo ametajwa kama Halyna Hutchins (42), ambaye alikuwa akifanya kazi kama mkurugenzi wa upigaji picha. Mtu anayetibiwa ni Joel Souza (48), mkurugenzi wa filamu.

Polisi wamesema bado wanachunguza tukio hilo huko Bonanza Creek Ranch, eneo maarufu la utengenezaji wa sinema, na hakuna mashtaka yoyote yaliyofunguliwa.

error: Content is protected !!