May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Staa Ligi Kuu England atua Bungeni

Mamadou Sakho akiwa na mkewe Bungeni Dodoma

Spread the love

 

Mlinzi wa kati wa klabu ya Crystal Palace ya nchini England Mamadou Sakho amefika Bungeni Jijini Dodoma na kuangalia shughuli za uwendeshaji wa chombo hicho. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezaji huyo amefika Bungeni leo tarehe 1 Juni, 2021 wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwenye kikao kilichongozwa na Spika Job Ndugai.

Sakho yupo nchini kwa siku 10 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za utalii akiwa pamoja na familia yake toka alipowasili tarehe 26 Mei, 2021 kufuatia kumalizika kwa Ligi Kuu nchini England ambapo klabu yake ilimaliza kwenye nafasi ya 14.

Mapema jana mchezaji huyo alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk Hussein Mwinyi na kukubaliana kufungua kituo cha michezo kitakacho wapa fursa vijana visiwani humo.

Rais Dk Hussein Mwinyi (kulia) akimkabidhi zawadi Mamadou Sakho (katikati) mara baada ya kumtembelea Ikulu visiwani Zanzibar

Mchezaji huyo mpaka sasa amefanikiwa kutembea vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Kijiji cha wamasai na seneto pamoja na visiwa vya Zanzibar.

error: Content is protected !!