
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne na upimaji wa kidato cha pili ambayo kwa ujumla yameonesha Shule ya Sekondari ya wasichana St. Francis imezidi kuzipiga vikumbo shule nyingine katika nafasi ya kwanza katika matokeo yote. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)
Katika matokeo hayo yaliyotangazwa leo tarehe 15, 2022 na Katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk. Charles Msonde yameonesha kuwa shule hiyo iliyopo mkoani Mbeya ndiyo iliyoongoza kitaifa katika mtihani wa kidato cha nne.
Aidha, katika matokeo ya upimaji wa kidato cha pili, vilevile Shule hiyo imekuwa ya kwanza huku ikiwa na idadi ya wanafunzi 92.
More Stories
Rais Samia afanya mapinduzi ya elimu Tabora, madarasa 74 yajengwa
Mbunge ataka nafuu wanafunzi wanaochanganyikiwa mtihani kidato cha nne
Rais Samia aokoa wanafunzi 271 kutoka ‘zizini’