July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

SSRA yatoa somo kwa watumishi

Spread the love

WANACHAMA wa mifuko ya hifadhi ya jamii wametakiwa kufuatilia makato yao kutokana na kuwepo kwa vitendo vya waajiri kuchelewesha upelekaji mafao hayo. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Mbali na hilo waajiri wametakiwa kutowalazimisha wafanyakazi wao kujiunga katika mfuko wasioupenda na badala yake wapewe nafasi ya kujieleza.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Ofisa Tehama (SSRA), Kenneth Batanyita alipokuwa akitoa elimu kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi mkoa wa Dodoma.

Amesema inasikitisha kuona baadhi ya waajiri wakiwalazimisha wafanyakazi wao kujiunga katika mifuko ambayo hawaitaki badala ya kuwapa nafasi ya wao kuchagua mifuko wanayoitaka.

Mbali na hilo amesema kutokana na kuwepo kwa waajiri ambao ni wasumbufu katika kupeleka makato ya wafanyakazi ni bora wafanyakazi wakawa wanafanya utaratibu wa kufuatilia kama makato hayo kama yanapelekwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa utafiti, Tathimini na Sera (SSRA), Ansgar Mushi, amewatoa hofu wanachama wa mifuko hiyo ya jamii kwa madai kuwa kamwe haiwezi kufa.

Aidha amesema mifuko hiyo ina malengo makubwa ya kuboresha maisha ya wastaafu pale wanapokuwa wamestaafu.

Naye katbu wa RAAWU mkoa wa Dodoma na Katibu wa TUCTA Kanda ya Kati, Ramadhani Mwendwa, amewataka wafanyakazi kujenga hoja pale wanapokuwa na madai yao badala ya kulalamika.

Amesema wafanyakazi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili lakini wanatumia muda mwingi kulalamika badala ya kujenga hoja.

error: Content is protected !!