Saturday , 13 April 2024
Home Habari Mchanganyiko SSRA: Dawa ya waajiri ‘wakaidi’ imepatikana
Habari Mchanganyiko

SSRA: Dawa ya waajiri ‘wakaidi’ imepatikana

Spread the love

HATUA ya waajiri kutolipa michango ya wafanyakazi wao katika mifuko ya kijamii imepatiwa dawa. Anaripoti Yusuph Katimba…(endelea).

Ilivyo sasa mwajiri akishindwa kulipa, atapelekwa Mahakamani na kisha atatakiwa kupeleka stakabadhi ya malipo ya michango ya mwajiriwa ama kumkana mwajiriwa.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya Msimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Onorius Njole.

Njole amesema hayo jana wakati wa kuwajengea uwezo wawakilishi wa vyombo vya habari jijini Dodoma.

“Mahakamani hakutakuwa na maneno mengie. Mwajiri atatakiwa kupeleka stakabadhi ama kumkana mwajiriwa wake basi,” amesema.

Pia amesema, kupunguzwa kwa mifuko ya Hifadhi ya Jamii kumetoa fursa ya kuwabana waajiri kwa kuwa hawana pa kukimbilia.

“Awali ilikuwa ukimbana mwajiri, anawatoa wafanyakazi na kuwapeleka mfuko mwingine lakini sasa hivi hakuna upenyo huo.

“Sasa kazi ya kudai michango ni ya mfuko nanmwajiriwa yeye hana kazi tena. Sheria inamlinda mfanyakazi,” amesema Njole.

Kwenye semina hiyo Mkurugenzi wa SSRA Dk. Irene Isaka amesema, ni marufuku kwa fedha za mafao ya wafanyakazi kutumika kulipa madeni, ambayo mwanachama aliingia wakati akiwa kwenye mazingira ya kufanya kazi.

Pia amesema kuna mpango kabambe wa serikali wa kulipa madeni ambayo ilikopa kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kabla ya kuunganishwa kwa mifuko hiyo.

Amesema hayo wakati akijibu maswali wakati wa semina ya kuwajenga uelewa wa Sheria mpya ya Hifadhi ya Jamii kwa Wahariri na Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali mjini hapa.

Dk Isaka amesema kulingana na sheria mpya ni marufuku kwa mafao ya mwanachama kutumika kulipa madeni ambayo mwanachama aliyaingia wakati akiwa kwenye mazingira ya uwezo wa kufanya kazi.

“Kwa sheria ya zamani kuna baadhi ya mifuko ilikuwa haizuii hili, lakini sasa mafao hayawezi kutumika kulipa madeni kwani lengo la mafao ni kumwezesha mwanachama kuendesha maisha yake pale ambapo uwezo wake wa kufanya kazi umepungua.”

Kuhusu malalamiko ya wanachama kujitoa, amesema hali hiyo haina tija na kuwa kwa sasa kutakuwa na Fao la Upotevu wa Ajira, ambalo litatolewa kwa mwanachama aliyefukuzwa kazi na si kwa yule aliyeamua kuacha kazi.

Kuhusu ulipaji wa madeni, amesema kwa sasa serikali imeanzisha Hati Fungani isiyo na malipo ambayo ndiyo itatumika kulipia madeni hayo.

“Niwahikishie wanachama kuwa serikali imeahidi kulipa fedha zote iliyokopa kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kabla ya kutekeleza sheria mpya ambayo imeunganisha mifuko na kuwa na mifuko mwili, mmoja wa watumishi wa umma na mwingine wa sekta binafsi,” amesema.

Amesema kwa sasa serikali haikopi tena kwenye mifuko hiyo baada ya kufikia ukomo wa asilimia 10 ya rasilimali ya mifuko na kuwa mara ya mwisho kukopa ilikuwa ni mwaka 2014.

Katika hilo Njole amesema kutokana na sheria hiyo, hakutakuwa na kodi yoyote kwenye mafao na michango ya mwanachama.

Alisema pia viwango vya uchangiaji bado vitabaki pale pale ambayo ni asilimia tano kwa mfanyakazi na 15 kwa mwajiri na kuwa hakutakuwa na fursa ya mwajiriwa kuchangia zaidi ya asilimia 10.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askofu ataka mafisadi, wauza mihadarati washughulikiwe kumuenzi Sokoine

Spread the love  MHASHAMU Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, Isaac...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mafuriko yaua 33 Morogoro, Pwani

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania imetoa tathmini ya athari ya mafuriko...

Habari Mchanganyiko

Wanafunzi 7 wahofiwa kufariki gari la shule likitumbukia korongoni

Spread the love  WANAFUNZI saba wanahofiwa kupoteza maisha, huku watatu wakinusurika katika...

Habari Mchanganyiko

Wazazi, walezi watakiwa kuwa karibu na watoto wao

Spread the love  WAZAZI na walezi wameagizwa kuwalea watoto wao katika maadili...

error: Content is protected !!