Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Spika Tulia: Sugu hanitishi, moto wangu anaujua
Habari za Siasa

Spika Tulia: Sugu hanitishi, moto wangu anaujua

Dk. Tulia Ackson
Spread the love

Spika wa Bunge, Tulia Ackson leo Alhamisi amesema licha ya kuwepo kwa chokochoko kwamba aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo kupitia Chadema, Joseph Mbilinyi ‘Sugu, Mr 2’ anampango wa kumng’oa katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025, mwanasiasa huyo hamtishi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Amesema wanaotaka kufahamu namna anavyokubalika kwa wananchi watembelee jimbo hilo kwani wanaoendekeza kauli hizo wanaishia kuzungumzia kwenye mitandao ya kijamii bila kuona uhalisia.

Pia amesema wanaotaka kugombea ubunge Mbeya Mjini wapime kina cha maji kama kinawatosha waingie kwenye kinya’ng’anyiro.

Spika Tulia ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini (CCM) ametoa kauli hiyo leo tarehe 4 Mei 2023 wakati wa mahojiano na kituo kimoja cha runinga nchini akiwa katika makazi yake Jijini Dodoma.

Amesema si kweli kwamba alishinda jimbo hilo kwa kubebwa na vyombo vya dola kwani sheria na taratibu kuhusu kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge zipo wazi na wapo wabunge waliowahi kufutiwa matokeo baada ya mpinzani wake kwenda mahakamani.

“Kama aliona ameonewa angeenda mahakamani kwa sababu sitaki kuamiani kama mahakama isingeteka haki,” Dk. Tulia.

Amesema kama alimgaraza mpinzani wake kabla halijawagawanya je, likigawanywa itakuwaje.

“Kama  likigawanywa, aje nilimtoa akiwa madarakani, sasa likigawanywa ninamuita njoo,” amesema Dk. Tulia.

Aidha, amesema sababu za kutaka jimbo hilo kugawanywa sio Mbeya Mjini pekee bali katika majimbo mbalimbali makubwa kwani uamuzi huo utasaidia kusogeza huduma karibu.

“Ubunge wangu haijalishi jimbo limegawanya au halijagawanywa, mimi ndio Mbunge kama nilimtoa mtu (Sugu) katika kata 36, hataweza kunitoa kata zikiwaa chache kweli? Mbona itakuwa mtihani, zikibaki kata 36 nitawafyeka.

“Nisingeshangaa kujadiliwa na wao, tena napenda sana wao wameanzisha huo mjadala nimefurahi na wanaposema watanifuata, nataka wajipime kama wanaona kina cha maji cha kinawatosha waje, kama niliwatoa na kata 36 wataniweza wapi na kata chache? amehoji Dk. Tulia.

Kauli hiyo ya Dk. Tulia imekuja siku moja baada ya jana Jumatano, Bunge kutaarifiwa kuwa kiongozi huyo ni miongoni wa wabunge waliowasilisha maombi ya kugawa majimbo yao ili kuwa mawili kutokana na ukubwa na wingi wa watu na hivyo kurahisisha shughuli za maendeleo.

Taarifa hiyo ilitolewa na bungeni na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Ummy Nderiananga, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Sophia Mwakagenda.

Swali la nyongeza kwa Serikali, Mwakagenda, aliuliza ni lini serikali italigawa jimbo la Mbeya mjini kutokana na ukubwa wake.

Aidha, baada ya kusambaa kwa taarifa hiyo, mjumbe wa kamati ya Chadema, Godbless Lema alisema hata jimbo la Mbeya Mjini likigawanywa watamfuata Dk. Tulia huko huko anapogombea.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 uliolalamikiwa na vyama vya upinzani, Dk Tulia alishinda kwa kura 75,225 dhidi ya Sugu 37,591 aliyeongoza jimbo la Mbeya Mjini kwa miaka 10 mfululizo kuanzia mwaka 2010/20.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!