July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Spika Tulia acharuka Mawaziri ‘watoro’ bungeni

Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson

Spread the love

 

SPIKA wa Bunge, Dk Tulia Ackson amewaagiza mawaziri waliopo bungeni kuwaita manaibu na mawaziri ambao hawahudhurii vikao vya Bunge licha ya kwamba wapo Dodoma.

Amesema mawaziri na manaibu mawaziri wote wanatakiwa wawepo wakati wote ambao wabunge wanajadili Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2022/2023. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akizungumza leo tarehe 16 Juni, 2022 Spika Dk. Tulia amesema katika mjadala huo wa bajeti kuu ya Serikali, zinajadiliwa hoja za kila wizara na kila wizara itapewa fursa ya kujibu hoja zake.

“Waheshimiwa mawaziri mliopo, muwape taarifa Naibu Mawaziri na Mawaziri waliopo Dodoma waje bungeni. Hoja ya Bajeti ni bajeti kuu ya Serikali na zinajadiliwa za kila wizara na kila wizara itapewa fursa ya kujibu hoja zake kwenye hoja hii.

“Kwa hiyo Mawaziri mliopo naomba muwaite mawaziri walioko Dodoma ambao hawana ruhusa ya kutokuwepo bungeni na lakini pia hawajasafiri na mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na hawajasafiri kwenda popote waje bungeni…kila mtu achukue hoja zinazomhusu,” amesema.

error: Content is protected !!