Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Spika Ndugai: Wakulima wanateswa na lumbesa
Habari Mchanganyiko

Spika Ndugai: Wakulima wanateswa na lumbesa

Gunia la viazi mviringo
Spread the love

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania, Job Ndugai amesema bado kuna tatizo kubwa katika vipimo sahihi wakati wa ununuzi wa mazao kutoka kwa wakulima licha ya kuwepo kwa Sheria ya vipimo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo ya Spika ilitolewa jana wakati akifungua Semina ya wabunge juu ya changamoto na mafanikio ya sheria ya vipimo ikiwa ni pamoja na wabunge hao kutoa michango yao katika semina hiyo jinsi ya kupambana na rushwa katika vipimo.

Wabunge hao ni wanachama wa hiari wa chama cha kupambana na vitendo vya rushwa APNAC ambao hutoa michango juu ya kupambana na rushwa na kuifikisha panapo husika.

Alisema wakulima wamekuwa wakinyonywa sana na baadhi ya wafanyabiashara kwa kutumia vipimo ambavyo si sahihi ikiwemo ufungaji wa mazao kwa njia ya lumbesa.

“Rasilimali nyingi zimekuwa zikipotea kutokana na ufungashaji kwa njia ya lumbesa na nyinginezo ambazo siyo rasmi tufikie wakati tuwe na sheria kali zaidi kwani wakulima wetu wamenyonywa  na kupunjwa vya kutosha,” alisema.

Akizungumzia kuhusiana na vipimo vya magari ya mizigo Spika alishangazwa kuona kuwa magari hayo licha ya kupita katika mizani mbalimbali lakini bado yanzuiwa sehemu fulani kwa sababu ya kutakiwa kupimwa tena.

Alisema hali hiyo imekuwa ikiwakera wananchi kwani hawaelewi nini tatizo mpaka kuwepo kwa vipimo kila sehemu na kufanya msururu wa magari kuwa mkubwa kusubiri kupimwa.

“Kama ni magari ya mizigo inawezekana wakaongeza njiani lakini kama wale wanaosafirisha mafuta kweli jamani tuliangalie na hilo tuliangalie,” alisema.

Alisema hali hiyo ni chimbuko la rushwa kwani kama mfanyabiashara anayesafirisha mafuta ameshapima vituo vyote hakuna sababu ya kumzuiakwani uwezekano wa kuongeza ujazo wa mafuta njiani ni mdogo.

Awali akitoa taarifa ya awali kwa wabunge wanachama wa chama cha wabunge wanapambana na rushwa (APNAC) Katibu wa APNAC Daniel Mtuka alisema APNEC iliundwa mwaka 2000.

Alisema madhumuni ya kuundwa kwake ni kupambana na rushwa mara baada ya kuona vitendo vya rushwa vinazidi.

Alisema wabunge waliokuwepo kipindi hicho waliona kuna umuhimu wa kuanzisha kikundi cha wabunge ambao watapambana na rushwa.

“APNAC  ilifanikiwa mwaka 2007 kushiriki kuandaa sheria namba 11 ya TAKUKURU ambapo sheria hiyo ilikuwa na vifungu vine tu lakini sasa vipo 24,” alisema

Alisema bado Sheria ya Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa inahitaji marekebisho zaidi. Alisema kutokana na hali hiyo APNAC ilita mawazo wakati wa mchakato wa Bunge la katiba ambao alisema ungewabana zaidi wanaokamatwa na vitendo vya rushwa.

“Tumeweza kutoa marekebisho mengi juu ya Sheria ya TAKUKURU na mengi yameweza kusaidia nchi yetu lakini bado tunaona ipo haja ya kuendelea kutoa mawazo yetu,” alisema Ndugai.

Kwa upande wa vipimo, Waziri wa Biashara na Viwanda, Josph Kakunda alisema bado kuna changamoto kubwa katika suala la vipimo.

Alisema kumekuwa na udanganyifu mkubwa kwa wafanyabiashara na madalali wanunuapo amzao toka kwa wakulima.

“Vipimo kama vya Lumbesa, Madebe na hata vikopo bado vimekuwa vikitumika katika sehemu nyingi hapa nchini ingawa tunavikataa,” alisema.

Alisema Wizara yake imeweza kujenga vituo vya msoko katika mipaka ili wakulima waweze kuuza mazao yao kihalali na uzito unaotakiwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!