Wednesday , 27 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Spika Ndugai: Wabunge wanadaiwa mabilioni, kulipa mashaka
Habari za Siasa

Spika Ndugai: Wabunge wanadaiwa mabilioni, kulipa mashaka

Spread the love

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai ameweka wazi kuwa wabunge kumi wa viti maalum waliokuwa wanatokana na chama cha CUF waliotimuliwa na chama hicho wanadaiwa zaidi ya Sh. 1 bilioni. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya mwenyendo wa mikopo kwa wabunge alisema kuwa wabunge wengi wanadaiwa fedha nyingi ambazo zinaweza kushindikana kulipwa na huenda deni hilo likalipwa na watanzania ambao ni walipa kodi.

Ndugai amelazimika kuwa wazi juu ya jambo hilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kuulizwa kuwa iwapo yeye ameweka wazi deni la Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), wabunge wa upinzani ambao walitimuliwa na CUF walikuwa na madeni na kama ndivyo walikuwa wakidaiwa kiasi gani.

Mbali na hilo aliulizwa kama wapo wabunge wengine ambao wanadaiwa au ni mbunge huyo tu ambaye anadaiwa fedha nyingi hivyo.

Akijibu maswali hayo alisema kuwa wabunge 10 wa Viti Maalum ambao walikuwa ni wabunge wa CUF wanadaiwa zaidi ya Sh. 1 bilioni na inaonesha wazi kuwa hawana uwezo wa kuzilipa.

Akizungumzia wabunge wengine ambao wanadaiwa alisema kuwa wabunge wengi wanadaiwa hata wale ambao wanajijiondoa katika ubunge wanaondoka na madeni jambo ambalo ni changamoto kubwa ndani ya bunge jambo ambalo linaweza kusababisha deni hilo kulipwa na watanzania ambao ni walipa kodi.

Kutokana na hali hiyo Spka alisema kuna haja sasa ya kuangalia uwezekano wa kubadilisha sera ya ndani ya fedha ndani ya Bunge ya kutowadhamini wabunge katika kupata mikopo na badala yake wajidhanini wenyewe.

Akizungumzia juu ya tukio la jana la kuweka zuio kwa wabunge kutofanya mahojiano na wabunge wa upinzani baada ya kutoka nje alisema ni kutokana na kuwepo kwa tabia ya wabunge kutoka nje kwa makusudi na kukimbiliwa na waandishi wa habari huku mijadala ikiendelea ndani ya Bunge.

Ndugai alisema kuwa licha ya kuwa mbunge yoyote hazuiliwi kutoka nje lakini imekuwa ni desturi ya wabunge wa upinzani kushindwa kuwa wavumilivu kwa kuwasikia wenzao wakichangia kwani mara kadhaa wamekuwa wakipewa nafasi ya kuchangia na wanapomaliza wamekuwa wakifanya fujo kwa kuzomea au kutoka nje.

Alieleza kwamba kinachotakiwa ni wabunge kuendelea kukaa ndani ya ukumbi wa bunge ili nao wasikilize hoja za watu wabunge wengine na waweze kujibu kwa hoja badala ya kukimbilia nje kwa kuzungumza na waandishi wa habari.

“Kwa mfano kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni anayo nafasi ya kuongea kwa muda wowote, Je ni kwanini awe ni mtu wa kutoka nje.

“Shida hapa ni kwamba wanashindwa kuzungumzaia ndani ya ukumbi wa bunge ambapo kuna kumbukumbu za kibunge wamekuwa wakizungumzia nje ya bunge ambapo hakuna kumbukumbu za bunge sasa hutamaduni huu siyo mzuri,” alisema Ndugai.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!