Friday , 1 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Spika Ndugai: Rais amesaini miswada sita
Habari za Siasa

Spika Ndugai: Rais amesaini miswada sita

Spread the love

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesaini miswada sita iliyopitishwa na Bunge la 11. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Miswada hiyo ni Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali namba 2 ya mwaka 2020, Muswada wa Sheria ya Mimea ya mwaka 2020, Muswada wa Sheria ya kusimamia na kuendeleza uvuvi wa bahari kuu 2020.

Muswada wa Sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali namba 3 2020, muswada wa Sheria ya Matumizi ya Fedha za Serikali ya mwaka 2020 na muswada wa mwisho ni Sheria ya Fedha 2020.

Taraifa hiyo imetoelewa leo Jumanne tarehe 16 Juni 2020 na Spika Job Ndugai, katika shughuli ya kufungwa kwa shughuli za Bunge la 11 jijini Dodoma.

“Kwa utendaji kazi wa rais wa namna ambayo isiyokuwa na ulinganifu, tayari ameshatia sahihi misiwada yote hiyo sita, ikiwa pamoja na ile sheria tuliyomaliza jana usiku saa 2 sheria ya fedha namba 8/2020, na yenyewe imetiwa saini tayari, kwenye kumbukumbu zetu miswada yote imepata kibali cha rais na ni sheria za nchi,” amesema Spika Ndugai.

Spika Ndugai amesema, kwa sasa miswada hiyo imekuwa sheria, ikiwemo Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali namba 2, sheria namba 3 ya mwaka 2020 , Sheria ya Afya ya Mimea namba 4 ya mwaka 2020.

Na Sheria ya Kusimamia na kuendeleza  uvuvi wa bahari kuu sheria namba 5 2020, na sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali namba 3 kifungu cha 6 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mwili wa Hayati Mwinyi kuagwa leo saa 8 Uwanja wa Uhuru

Spread the loveMWILI wa Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi unatarajiwa kuagwa kuanza...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari za Siasa

Waziri mkuu Ethiopia atua Tanzania

Spread the loveWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,...

error: Content is protected !!