January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Spika Ndugai: Nimekosa mimi, nimekosa sana, nisameheni

Aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai

Spread the love

 

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amemwomba radhi, Rais Samia Suluhu Hassan na Watanzania wote waliokwazika kutokana na kauli aliyoitoa kuhusu serikali kuendelea kukopa fedha za kugharamikia miradi ya maendeleo. Anaripoti Danson Kaijage, , Dodoma … (endelea).

Spika Ndugai ameomba radhi kipindi ambacho kumekuwa na matamko mbalimbali kutoka ndani ya chama chake huku wengine wakienda mbali zaidi kwa kumtaka kujiuzulu.

Ni baada ya kueleza kwamba Serikali inayoongozwa na Rais Samia imeendelea kukopa na madeni yakiendelea na kuwa makubwa kuna hatari ya nchi kupigwa mnada.

Kauli hiyo ilimuibua Rais Samia aliyesema, Serikali itaendelea kukopa kugharamikia miradi ya maendeleo huku viongozi wengine waandamizi wa serikali nao wakitetea serikali kukopa.

Chama Cha Mapinduzi ngazi ya mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Singida, Kilimanjaro, Njombe na Umoja wa Vijana (UVCCM), ulimpinga Ndugai na kusimama na Rais Samian a kumtaka kumwacha Rais atekeleze majukumu vyema.

Leo Jumatatu, tarehe 3 Januari 2022, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake bungeni jijini Dodoma, Spikja Ndugai amesema, ujumbe wake hakukuwa na lolote la kudharau juhudi za serikali inayoongozwa na Rais Samia kwani “serikali ni baba yetu na mama yetu, tunahitaji serikali na tunaiunga mkono na niliwataka wenzangu kujiimarisha kiuchumi, tulipe kodi na tozo, huo ndiyo ulikuwa msisitizo wa hotuba yangu.”

Amesema, watu walikata baadhi ya mambo kwenye ujumbe wake alipokuwa anazungumza kwenye mkutano mkuu wa umoja wa Wagogo uliofanyika mwishoni mwa Desemba 2021, wakawasilisha ujumbe nusu, ujumbe huo ndio umeibua mjadala mkubwa katika nchi yetu na kusababisha usumbufu.

“Popote pale ambapo niliteleza naomba nitumie fursa hii kumwomba radhi Rais Samia na Watanzania,” amesema Spika Ndugai.

Amesema, chini ya utawala wa Rais Samia, “nchi imetulia, iko salama katika mikono ya Mama Samia, kilichotokea ni kitu cha kutengeneza tu lakini hakuna ukweli.”

Kuhusu waliomtolea kauli na maneno mbalimbali wakiwemo vijana na kumwaza, “niwaombe radhi na mimi ni yuleyule. Nimekosa mimi, nimekosa sana. Mungu anisamehe. Watanzania nisameheni sana.”

Spika Ndugai amesema, “nitakuwa nimebeba dhambi kubwa nikiwa namkatisha mama tamaa kwetu Kongwa tumepata fedha nyingi haijawahi kutokea na sisi tumeezekea mabati ya kijani nagumu siyo yale ya sufuria.”

error: Content is protected !!