Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Spika Ndugai: Nilimchapa viboko mpinzani wangu
Habari za SiasaTangulizi

Spika Ndugai: Nilimchapa viboko mpinzani wangu

Job Ndugai akiwa jukwaani katika uchaguzi wa mwaka 2015. Picha ndogo Dk. Joseph Chilongani aliyechapwa viboko na Ndugai
Spread the love

SPIKA wa Bunge la Jamhuri, Job Ndugai, amekiri kumshambulia kwa fimbo Dk. Joseph Chilongani, ambaye aliyekuwa mmoja wa washindani wake wenye nguvu wakati wa kinyang’anyiro cha kuwania kuteuliwa kuwa mgombea ubunge ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Ndugai alitoa ushuhuda huo leo Alhamisi, bungeni mjini Dodoma, kufuatia kuibuka kwa mjadala mzito juu ya matumizi ya adhabu ya viboko kwa wanafunzi wa shule za msingi.

Alisema, suala la adhabu ya vikobo, ni muhimu sana kwa kuwa hata mimi niliwahi kumchapa mtu viboko na kwamba miongoni mwa makabila ya wamasai na Wagogo, kuchapa viboko ni suala la kawaida.”

Hata hivyo, kauli ya Spika Ndugai ya kutaka kuhalalisha viboko inapingana na kinachoonekana kwenye mkanda wa video, uliyonakiri tukio hilo.

Kwa mujibu wa mkanda wa video unamuonyesha Spika Ndugai akimshambulia Dk. Chilongani, kunaonekana baadhi ya wazee wa kabila la Kigogo, pamoja na akina baadhi ya wanawake, wakilalamikia kitendo hicho.

Aidha, ndani ya mkanda huo wa video, baadhi ya waliokuwapo walionekana kuhuzunishwa na tukio hilo, huku wengine wakimzuia Ndugai kumshambulia Dk. Chilongani.

Ndugai alimtuhumu Dk. Chilongani kumpiga picha, mara baada ya spika huyo wa Bunge kuanza kufanya vurugu kwenye mkutano wa kampeni wa kura ya maoni kwa kile alichodai kuwa mshindani wake alikuwa anampiga picha.

Katika mjadala huo wa bungeni, baadhi ya wabunge walipinga adhabu hiyo na kuitaka serikali kutafuta adhabu mbadala na kuacha suala la viboko kwa wazazi, huku wengine wakitaka iendelee ili wanafunzi wawe na nidhamu.

Akijibu kuhusu mjadala huo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, alisema kuwa utoaji adhabu ya viboko kwa wanafunzi unalenga kuimarisha nidhamu hasa kwa watoto wasiofuata sheria.

Prof. Ndalichako amewataka walimu kutumia taratibu stahiki wanapotoa adhabu hiyo.

“Niongelee hili suala, suala la utoaji viboko lengo lake sio kuongeza ufaulu bali kurekebisha dosari zilizjitokeza, suala la adhabu hutolewa pale mtu anapokiuka taratibu.

“Nitumie fursa hii kuwashauri wanafunzi kutii sheria bila shuruti, pale inapokuwa na ulazima pindi mwananfunzi anapokiuka kutumia taratibu za adhabu zilizowekwa na akienda kinyume ataadhibiwa,” amesema Prof. Ndalichako.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!