January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Spika Ndugai kuwekewa pingamizi

Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai

Spread the love

WAGOMBEA ubunge jimbo la Kongwa kupitia (CCM), kwa ujumla wao wameandika barua ya pingamizi kwa Mkurugenzi wa uchaguzi mkoa Dodoma kwa lengo la kupinga matokeo iwapo atatangazwa kuwa mshindi katika kura za maoni. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Akizungumza kwa niaba ya wenzake Samuel Chimanyi akizungumza na waandishi wa habari alisema wagombea hao wamelazimika kuandika barua hiyo kutokana na mgombea mwenzao kuwachezea rafu za wazi wazi

Jambo ambalo wagombea hao wana lalamikia ni kitendo cha ndugai kuendeleza kucheza rafu katika uchaguzi huku uongozi wa mkoa CCM na Wilaya wakinyamaza kimya.

Chimanyi amesema yapo mambo mengi ambayo yanaonekana kufanywa na ndugai ambayo kwa ujumla yanaonesha wazi ni kufanya kampeini kwa kuvunja kanuni na taratibu.

Msemaji huyo amesema katika hali isiyokuwa ya kawaida vipo vituo ambavyo vinaonekana kuwa na idadi kubwa katika upigaji kura wakati idadi halisi ni ndogo.

Licha ya kuwepo kwa vituo ambavyo vina idadi kubwa ya wapiga kura tofauti na idadi ambayo ipo katika daftari la kujiandikisha la CCM, bado kuna vitendo vya rushwa ambavyo vilikuwa vikifanyika wazi wazi.

Wagombea hao ambao idadi yao ni sita kati ya tisa walisahini barua hiyo ambayo nakara yake imepelekwa kwa Kamati ya Maadili Taifa,Katibu Mkuu wa CCM Taifa na katibu wa CCM wilaya ya Kongwa.

Kutokana na hali hiyo Chimanyi alisema kama uongozi wa CCM kwa ngazi yoyote hile hautakuwa tayari kumwajibisha Ndugai kutokana na kuvunja kanuni na taratibu za CCM ni wazi kwamba watajivua uanachama.

“ Hatuwezi kuvumilia kuona chama kinidharirishwa huku viongozi wakiwa kimya, Ndugai kafanya kampeini chafu na katoa rushwa za wazi wazi.

“ Katika semina iliyotolewa na Taasisi ya Kuzuia na na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) tuliambiwa hakuna mtu yoyote ambaye anaruhusiwa kutoa zawadi katika kipindi chote cha kampeini za kura za maoni, lakini kwa Ndugai imekuwa kinyume.

“Katika kuendelea na kampeini bila kujali kuwa kanuni zinakataza Ndugai alitoa fedha hadaharani kwa uongozi wa kanisa kwa madai kwanba bni ahadi yake ya siku nyingi.

“Hiyo kama haitoshi aliweza kuwanunulia akina mama wa CCM ambao ni wapiga kura wakati wa uchaguzi wa kura za maoni wa wabunge wa viti maalum kwa kuwanunulia maji jambo ambalo ni kinyume na kanuni za sheria ya uchaguzi” alisema Chimanyi.

Kwa ujumla wagombea hao kwa pamoja walisema kamwe hawaezi kukubaliana na matokeo ya aina yoyote ambayo yatatangazwa na mkurugenzi wa uchaguzi kwani kuna ubabaishaji mkubwa.

Alipoulizwa Karibu wa CCM mkoa Albert Mguma alipoulizwa kama kweli kapata barua hiyo ya malalamiko kutoka kwa wagombea amesema yeye hausiki na badala yake anapatiwa nakala ya malalamiko.

“Mimi napatiwa nakala ya barua ya malalamiko hivyo sijui kama kweli hiyo barua hipo mezani kwangu licha ya kuwa nimewaona hapa maeneo ya ofisini, lakini ebu jaribu kuwasiliana na katibu wa CCM wilaya ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi.

Kwa upande wake msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Kongwa Masimami Javan alisema yeye hawezi kuzungumza jambo lolote kwani msemaji ni Katibu wa Wilaya ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi.

Katika hatua nyingine Chimanyi kwa niaba ya wagombea wenzake alisema wanatoa siku tatu kuhakikisha Ndugai anafikishwa mahakamani na ikishindika watafanya maandamano na sambamba na kushinikiza kufunguliwa kesi ambayo inaonekana kusuasua.

“Tunajenga mashaka na uongozi wa jeshi la polisi pamoja na uongozi wa CCM wilaya na Mkoa haiwezekani kila malalamiko ambayo yanatolewa na walalamikaji wanajikuta kama wanatwanga maji kwenye kinu” amesema Chimanyi.

Hata hivyo alipotafuta Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, David Misime alipoulizwa kama Job Ndugai ameishafikishwa mahakamani kutokana na kauli yake kuwa jalada lake lipo tayari hakuweza kulizungumzia jambo hilo na badala yake amesema taarifa hizo zitafutwe mahakamani.

Alipotafutwa mlalamikiwa ambaye ni Job Ndugai ili aweze kuelezea tuhuma zinazomkabili hakuweza kupatikana kwani simu yake ya kiganjani ilikuwa ikiita bila kuwa na mafanikio.

error: Content is protected !!