July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Spika Ndugai kufikishwa mahakamani

Naibu Spika na Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Job Ndugai akizungumza kwenye mkutano wa hadhara jimboni kwake

Naibu Spika na Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Job Ndugai akizungumza kwenye mkutano wa hadhara jimboni kwake

Spread the love

JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma limesema kwamba limeisha kamilisha jalada la kumshitaki Naibu Spika Job Ndugai kutokana na kumpiga mgombea mwenzake wa CCM, Dk. Joseph Chilongani. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Akizungumza Mwanahalisione Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma David Misime amesema kwamba jeshi hilo limechukua uamuzi huo kutokana na mlalamikaji kutoa taarifa katika kituo cha polisi na kuandika maeelezo ya kupigwa kwake.

Amesema baada ya kupigwa Dk .Chilongani alienda katika kituo cha polisi wilayani Mpwapwa na kutoaa maelezo na kupatiwa PF3 kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Misime amesema jeshi la polisi liliweza kumkamata Ndugai lakini alijidhamini kwa mali yake mwenyewe na kutokana na hali hiyo jeshi la polisi limeisha kamilisha uandaaji wa jalada la mashitaka ambalo litapelekwa kwa mwana sheria wa serikali kwa ajili ya kwenda mahakamani.

“Jeshi la polisi limeisha fanya taratibu zake baada ya mlalamikaji kufika katika kituo cha polisi na alipatiwa PF3 kwa ajili ya matibabu ,na baada ya hapo alitafutwa mtuhumiwa abaye ni Job Ndugai nayealitoa maelezo yake na kujidhamini kwa mali zake.

“Kutokana hali hiyo jeshi la polisi limeweza kukamilisha jarada la mshitaka ambalo litaperekwa kwa mwana sheria wa serikali ili hatua nyingine za kisheria kufuatia ziweze kukamilika sisi tumeisha kamilisha taratibu zote, tunasubiri ripoti ya daktari ambaye alimtibu Dk. Chilongani ili tuwezekuambatanisha na tumkabidhi mwana sheria wa serikali ili awezekufanya majukumu yake,” amesema Misime.

Mbali na hilo Misime amesema jeshi la polisi linafanya kazi zake kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu na halitaweza kumuonea mtu yeyote kulitokana na hela zake, umaarufu na badala yake kazi itafanyika kwa ueledi mkubwa.

Kuandaliwa kwa jarada hilo kunatokana na Job Ndugai kumshabulia mgombea mwenzake Dk.Chilongani ambaye alipigwa na kuzimia hadi kufikia hatua ya kulazwa katika hospitali ya wilaya ya Kongwa.

Hata hivyo wagombea wenzake na Ndugai wametishi kujiengua CCM aiwapo kamati ya nidhamu ya CCM taifa haitamchukulia hatua kali za kinidhamu Job Ndugai kutokana navitendo vya uvunjaji wa sheria na kanuni.

Akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa wagombea Samuel Chimani amesema Ndugai amekuwa kinala mkubwa wa uvunjifu wa maadili ndani ya chama.

error: Content is protected !!