Sunday , 26 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Spika Ndugai: CCM ilitaabika uchaguzi mkuu 2020
Habari za Siasa

Spika Ndugai: CCM ilitaabika uchaguzi mkuu 2020

Spika Job Ndugai
Spread the love

 

JOB Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania, amelieleza Bunge, katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, Chama Cha Mapinduzi (CCM), ‘kilitoka jasho.’ Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Amesema, suala la wanawake kutozwa fedha wakati wakijifungua, lilikiweka chama hicho katika wakati mgumbu mbele ya wananchi.

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo bungeni leo Alhamisi tarehe 11 Februari 2021, baada ya swali la nyongeza la Hawa Mwaifunga, Mbunge wa Viti Maalum, asiyekuwa na chama baada ya kufukuzwa Chadema ambaye ametaa kujua kama serikali inatambua kuna hospitali wanatoza wananawake wanaojifugua.

Mbunge huyo amefafanua, kwamba kwa wanawake wanaojifungua watoto wa kiume hutakiwa kulipa Sh50,000 na Sh40,000 kwa wanaojifungua watoto wa kike.

Swali hilo limemgusa Spika Ndugai ambaye ameitaka serikali kuangalia kwa upana wake ssuala hilo, akitolea mfano wa ukubwa wa tatizo hilo Tabora.

Spika Ndugai amesisitiza kwamba, kinachozungumza wabunge kuhusu tozo hizo kwa wazazi, kina ukweli na kilionekana wazi wakati wa kampeni za uchaguzi kuu 2020.

“Watu wa Serikali naomba mlitazame maana lilitusumbua sana kwenye kampeni na sasa mkoani Tabora, jambo hilo lazima mlitazame kwa namna yake,” amesema Spika Ndugai.

Grace Tendega, Mbunge wa Viti Maalum ambaye naye alifukuzwa Chadema, awali katika swali la nyongeza, alitaka kujua kwanini watumishi wa afya wanawatoza wajawazito wanaojifungua nje ya vituo vya afya kati ya Sh50,00O hadi Sh70,000.

Hata hivyo, Dk Festo Ndugange ambaye ni Naibu Waziri wa Tamisemi amesema, serikali haijatoa kauli ama kubadili msimamo kuwa wanawake wanaojifungua nje ya vituo, kutozwa fedha kiasi hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!