April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Spika Ndugai: Bunge halina ugomvi na Ofisi ya CAG

Prof. Mussa Assad, Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali. Picha ndogo Job Ndugai, Spika wa Bunge

Spread the love

JOB Ndugai, Spika wa Bunge ameeleza kwamba, taasisi anayoiongoza haina ugomvi na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), bali lina ugomvi na mtu (Prof. Mussa Assad). Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Amesema, ameamua kutoa ufafanuzi huo kutokana na redio moja nchini kutoa habari za kupotosha kwamba, Bunge limegoma kufanya kazi na Ofisi ya CAG.

Maswali yamekuwa yakiibuliwa kwamba, ni kwa namna gani Bunge linaweza kufanya kazi na Ofisi ya CAG bila maofisa wa ofisi hiyo kupata maelekezo kutoka kwa mkuu wa taasisi hiyo, Prof. Assad.

Miongoni mwa waliohoji swali hilo ni Askofu Benson Bagonza, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Karagwe ambaye amehoji; “Bunge limepitisha kutofanya kazi na Prof. Assad au CAG?”

Na kwamba, kama Bunge limegoma kufanya kazi na Prof. Assad ambapo Rais John Magufuli siku chache zijazo atapeleka ripoti ya mkaguzi isomwe bungeni, akiipeleka atakuwa amelidharau Bunge na akiacha atakuwa amevunja katiba.

Hata hivyo, Prof. Assad akizungumza na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) alisema, Bunge linapaswa kupitia uamuzi wake kwa kuwa, unaweza kusababisha mgogoro mkubwa kinyume na inavyoonekana sasa.

error: Content is protected !!