Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Spika Ndugai awapiga ‘stop’ wabunge 15 Chadema, akiwamo Mbowe 
Habari za SiasaTangulizi

Spika Ndugai awapiga ‘stop’ wabunge 15 Chadema, akiwamo Mbowe 

Spread the love

JOB Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametoa orodha ya wabunge 15 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutekeleza maagizo yake mawili iwapo wanataka kurejea bungeni. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kati ya wabunge hao 15 wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania, yumo Freeman Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Uamuzi huo wa Spika Ndugai ameutoa leo Jumatano tarehe 13 Mei 2020 kupitia taarifa  yake kwa umma juu ya wabunge hao waliojiweka karantini kwa siku 14.

Tarehe 1 Mei 2020, Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema alitoa maagizo ya chama hicho ya kuwataka wabunge wake kujiweka karantini ili kuangalia kama wameambukizwa virusi vya corona ama la!

Pia, Mbowe alitoa ushauri kwa uongozi wa Bunge kusitisha shughuli za Bunge la Bajeti linaloendelea na kujiweka karantini ikiwamo kuwapima wabunge na watumishi wote wa muhimili huo maambukizo ya corona.

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema

Hata hivyo, Spika Ndugai alipinga uamuzi huo akisema shughuli za Bunge zitaendelea bila kusimama huku akiwataka wabunge hao kurejea bungeni lasivyo watachukuliwa hatua.

Katika taarifa yake kwa umma, Spika Ndugai amesema katika siku za hivi karibuni baadhi ya wabunge wa Chadema wamekuwa watoro kwo kutohudhuria vikao vya Bunge bila ruhusa ya Spika kwa muda wa wiki mbili kinyume na masharti ya Kanuni ya 146 inayosisitiza wajibu wa kila mbunge kuhudhuria vikao vya Bunge.

Aidha, tunapenda ifahamike kwamba wabunge hao walisusia vikao vya Bunge huku wakiwa wamelipwa posho ya kujikimu ya kuanzia tarehe 1-17 Mei, 2020.

Kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 5 ya Kanuni za Bunge, Spika Ndugai alitoa masharti mawili kwa wabunge hao kama ifuotavya; kuwataka kurejea bungeni au kurudisha fedha walizolipwa mara moja.

Pili, kwa kuwa haijulikani wabunge hao walipo, watalazimika kuwasilisha ushahidi kwamba wamepimwa na hawana maambukizi ya virusi vya Covid-19 kabla ya kuruhusiwa kuingia Bungeni.

Amewataja wabunge hao na majimbo yao kwenye mabano ni; Freeman Mbowe (Hai), Ester Bulaya (Bunga Mjini), Halima Mdee (Kawe), John Heche (Tarime Vijijini), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu (Mbeya Mjini), Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini), Pascal Haonga (Mbozi) na Joseph Haule maarufu Profesa J wa Mikumi.

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akitafakari jambo bungeni

Wengine ni; Rhoda Kunchela, Catherine Rage, Devotha Minja, Joyce Mukya, Aida Joseph Khenan, Upendo Peneza na Grace Kiwelu wote wa viti maalum.

“Hivyo basi, kwa taarifa hii, na kwa mujibu we Kanuni ya 144 ya Kanuni za Kudumu za Bunge inayohusu usalama katiko maeneo ya Bunge. Spika ameagiza Kitengo cha usalama cha Bunge kutowaruhusu wabunge waliotajwa kutoingia bungeni kuanzia leo JUmatano tarehe 13 Mei 2020 mpaka watakapotimiza masharti tajwa hapo juu,” amesema Spika Ndugai kwenye taarifa yake

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!