SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewaapisha Humphrey Polepole na Riziki Lulinda kuwa wabunge wa Bunge hilo. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).
Polepole na Riziki wameapishwa leo Jumatatu tarehe 30 Desemba 2020 Viwanja vya Bunge jijini Dar es Salaam.
Wawili hao, wameapishwa baada ya Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli jana Jumapili kuwateua kuwa wabunge katika nafasi zake kumi za wabunge.
Polepole anaingia kwa mara ya kwanza bungeni huku Riziki yeye anarejea kwa mara nyingine kwani katika Bunge lililopita alikuwa mbunge wa viti maalum kupitia Chama Cha Wananchi (CUF).
Mwishoni mwa mkutano wa Bunge la 11, Riziki alitangaza kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM) alikokuwa akihudumu kabla ya kutimkia CUF.

Akizungumza baada ya kuaoishwa, Riziki amemshukuru Rais Magufuli kwa kumteua pamoja na wananchi wa Lindi kwa maombi yake.
Polepole ambaye pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM amesema, “namshukuru Mungu wa binguni ambaye yeye imempendeza Rais anipe jukumu hili ili kuwasaidia umma wa Watanzania wanapata maendeleo.”
Amesema, “sisi tutamsaidie Rais John Magufuli kutekeleza yale yaliyoahidiwa. Naahidi kuwa mwaminifu na mtiifu na nitakuwa tayari kujifunza.”
Leave a comment