Saturday , 10 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Spika Ndugai ataka Ma-RC wabanwe
Habari za SiasaTangulizi

Spika Ndugai ataka Ma-RC wabanwe

Rais Samia Suluhu Hassan akimuapisha Queen Sendiga kuwa Mkuu wa mkoa wa Iringa
Spread the love

 

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ameshauri wakuu wa mikoa (RC), wawajibishwe mikoa yao inapofanya vibaya katika usimamizi wa masuala ya fedha, badala ya kuwajibishwa wakurugenzi peke yake. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Spika Ndugai amesema hayo leo Jumatano, tarehe 19 Mei 2021, Ikulu jijini Dar es Salaam, akizungumza katika hafla ya uapisho wa wakuu wa mikoa na wakuu wa taasisi walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, hivi karibuni.

“Haiwezekani rais ameweka maelekezo asilimai 40 ya bajeti za mikoa iende kwenye maendeleo, zinakuja halmashauri bungeni hata asilimia 10 au 20 hazijafika au 60 ya majiji halafu mkuu wa mkoa anashangaa bungeni kwamba hazijatengwa. Mimi ushauri wangu uwajibikaji uwe wa pande zote,” amesema Spika Ndugai.

         Soma zaidi:-

Amemtaka, Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Ummy Mwalimu, aufanyie kazi ushauri huo.

“Ummy yuko hapa sisi pendekezo letu, hebu tuweze mzunguko wa uwujibikaji kati ya wakuu wa mikoa, wilaya na mkurugenzi, kama hawatekelezi vizuri wawajibike wote. Kama akiwajibishwa mkurugenzi peke yake wegine wanarelalax,” amesema Spika Ndugai.

Amesema katika maeneo ambayo uongozi wa mikoa inafanya vibaya ni pamoja na utekelezaji wa bajeti za ofisi zao, utoaji wa asilimia 10 ya mapato ya mikoa hiyo kwa ajili ya mikopo kwa kina wanawake, vijana na walemavu.

“Tunapokutana nao baadhi yao hasa kamati yetu ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, baadhi yao mambo wanayoelezwa kuhusu halmashauri zao au wilaya na wao wanakuja kushangaa pale bungeni. Nadhani hili niwaleeze haipendezi unakuja kushangaa vitu vya kwako mwenyewe,” amesema Spika Ndugai.

Job Ndugai, Spika wa Bunge la Tanzania

Spika Ndugai amesema “kama sheria itungwe aislimia 10 ya fedha iende kwa wanawake halafu inakuja halmashauri kadha ndani ya mkoa ule haijatengwa, halafu ukiuliza anasema tumuulzie mkurugenzi haiwezekani.”

Spika Ndugai amewataka viongozi hao wa mikoa kutotumia madaraka yao vibaya.

“Wapo wakuu wa wilaya huko nyuma sio ninyi wanaamini kabisa wao kule waliko ni rais, utasikia mimi rais wa mkoa huu au wa wilaya hii nani amesema? Rais ni samia Suluhu Hassan, huo ndio ukweli usije ukajidanganya wewe ndiyo rais,” amesema Spika Ndugai.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

MichezoTangulizi

Benki ya NBC yakabidhi kombe la ubingwa wa ligi kuu kwa Yanga

Spread the loveMDHAMINI Mkuu wa ligi ya NBC, Benki ya Taifa ya...

BiasharaTangulizi

TLS wajitosa sakata la ukodishaji wa bandari

Spread the love  CHAMA cha wanasheria Tanzania (TLS), kimejitosa katika sakata la...

BiasharaTangulizi

Ngoma bado mbichi mkataba wa Bandari

Spread the love  SAKATA la mkataba wa uendeshaji, uendelezaji na uboreshaji wa...

BiasharaTangulizi

Mkurugenzi TPA: Mkataba unaweza kuvunjwa

Spread the loveMKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA),...

error: Content is protected !!