April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Spika Ndugai ‘anyonga’ swali la Mbunge Chadema

Job Ndugai, Spika wa Bunge la 12 la Tanzania

Spread the love

SWALI la papo kwa papo Kasim Majaliwa, Waziri Mkuu kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa, ‘limenyongwa’ juu kwa juu na Job Ndugai, Spika wa Bunge. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Devotha Minja, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), wakati akianza kutoa maelezo kuhusu swali lake, Spika Ndugai alimzuia kuendelea kwa maelezo, kanuni za Bunge hazirihuru ‘kuandikiwa swali.’

Leo tarehe 14 Novemba 2019, Minja alianza kutoa maelezo kuhusu hila na hujuma zinazofanywa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mbunge huyo alijikita kwenye kauli zilizotolewa na Seleman Jafo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Mwita Waitara, Naibu Waziri wa TAMISEMI.

Mwelekeo wa swali la Minja kabla ya kuuliza swali lenyewe, ulikiutana na kigingi cha Spika Ndugai, na kujikuta akitupwa nje na nafasi ya kuuliza kupewa mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Hilo swali si lako, umeandikiwa na waliokutuma,” aliambiwa Minja ambaye naye alijibu “sijaandikiwa.”

Spika Ndugai alihama kwa Minja na nafasi hiyo kumpa Allan Kiula,

Mbunge wa Mkalama (CCM), ambaye alijikita katika hofu kuhusu haki ya kupiga na kupigiwa kura katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 24 Novemba 2019.

Hata hivyo, Waziri Majaliwa alisisitiza kuzingatiwa kwa sheria, kanuni na taratibu katika kutimiza azma ya kuchagua viongozi kwenye uchaguzi huo.

error: Content is protected !!