JOB Ndugai, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema, mbunge aliyekuwa aliyeambukizwa virusi vya corona (COVID-19), ataruhusiwa mda wowote kutoka sasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).
Amesema, mbunge huyo (bila kumtaja jina wala jimbo analotoka), anasubiri kufanyi wa vipimo vya mwisho ili aruhusiwa na hatimaye kuungana na familia yake.
“…hali ya mbunge wa kwanza aliyetangazwa kuwa na maambukizi ya Virusi vya Corona, inaendelea vizuri na kwamba hana dalili zozote za maambukizi hivyo anangoja vipimo vya mwisho ili aweze kuruhusiwa,” amesema Spika Ndugai.
Wiki mbili zilizopita, Dk. Tulia Akson, Naibu Spika wa Bunge, alilitangazia Bunge kuwa mmoja wa wabunge wa Bunge hilo, amepatwa na virusi vya corona.
Leave a comment