May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Spika Ndugai ampa somo CAG

Spread the love

 

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, imetaka Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali, kujikita katika kuandaa ripoti za ufanisi ili kupata picha juu ya utendaji wa watumishi ndani ya serikali. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Ndugai, aliyasema hayo jana Ijumaa, tarehe 2 Julai 2021, jijini Dodoma wakati alipokuwa akitoa hotuba yake kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya ofisi hiyo toka kuanzaishwa kwake.

Alisema hivi sasa ipo haja kwa ofisi hiyo kuanza kujikita katika kuanda ripoti za ukagauzi wa ufanisi katika maeneo mbalimbali.

“Ni wakati sasa mnaandaa ripoti hizi za kihasibu lakini pia muanze kuandaa ripoti zinazaohusu ufanisi ili kuondoa malalamiko yanayotoka kwa wananchi,” alisema Ndugai.

Job Ndugai

Aidha, alisema kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa pamoja na ofisi hiyo kutoa hati safi lakini bado kuna vitu vinaoneka kuwa haviko sawa.

“Wananchi bado wanalalamika unakuta halmashauri inapewa hati safi lakini wakiangalia hakuna kitu ambacho kipo sawa, hivyo ripoti hizi za ufanisi zitasadia kuondoa malalamiko haya kwa kupima utendaji wa watumishi,” alisema Ndugai

Pia, alisema Bunge litaendelea kushirikiana na ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali katika kujadili ripoti zinazowasirishwa kwa maslahi ya taifa.

Alisema ripoti ya mkaguzi mkuu wa Serikali ni nyenzo muhimu sana kwa Bunge inayolisaidia kuhoji na kuisimamia serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Pia, tunaomba ofisi yako CAG, kuendelea kutoa elimu kwa waheshimiwa wabunge wetu ili kuwa na mbinu bora za kuhoji mambo mbalimbali katika maneo yao na kuisaidia serikali yetu na Rais wetu” alisema.

Charles Kichere, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)

Kadhalaia aliomba ofisi hiyo kutoa mafunzo kwa wahasibu hasa wa Ofisi ya Rais Tamisemi ambao kwa kiasi wapo nyuma kutoka na kukosa mafunzo ya mara kwa mara.

“Mnaweza mkawa mnawahusu wahasibu wetu kwa kufanya vibaya katika maheasabu lakini ukweli ni kwamba wapo nyuma hasa wale wa Tamisemi hawapati mafunzo ya mara kwa mara”alisema

Kwa upande wake, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere, alisema wanaishukuru serikali kwa kuendelea kuiwezesha kutekeleza majukumu yake kwa kuipatia fedha pamoja na rasimali watu.

Vile vile, Kichere aliliomba Bunge kubadili muda wa kujadili ripori yake anayoiwasairisha bungeni katika mwaka wa fedha husika tofauti na ilivyo sasa ambapo inajadiriwa mwaka unaofuata.

Hata hivyo, alisema lengo la ofisi hiyo ni kuwa taasisi ya kisasa kwa kuipindi chake cha uongozi.

error: Content is protected !!