Friday , 2 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Spika Ndugai amng’ang’ania Lema
Habari za SiasaMpya

Spika Ndugai amng’ang’ania Lema

Job Ndugai, aliyekuwa Spika wa Bunge Tanzania
Spread the love

GODBLESS Lema, Mbunge wa Arusha Mjini leo mchana tarehe 3 Aprili 2019 atakutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maadili saa 8 mchana baada ya kuagiza kufanya hivyo na Job Ndugai, Spika wa Bunge. Anaripoti Danson Kaijage…(endelea).

Spika Ndugai ametoa agizo hilo muda mfupi baada ya kufanya utambulisho wa wageni waliofika bungeni hapo. Kabla ya kutoa maagizo hayo alisema “nina tangazo fupi juu ya kilichotokea jana.”

 Amesema, tangazo lake linahusu kauli ya Lema iliyounga mkono kauli ya Halima Mdee, Mbunge wa Kawe ambaye aliunga mkono kauli ya Prof. Mussa Assad, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwamba, Bunge ni dhaifau.

 Jana tarehe 2 Aprili 2019, baaday ya mjadala wa ripoti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maadili kuwasilishwa, katika uchangiaji wake Mdee aliungana na kauli ya Prof. Assad kwamba, Bunge ni dhaifu na kusababisha kupewa adhabu ya kutohudhuria vikao viwili vya Bunge.

 Spika Ndugai amesema, “nadhani wote mnafahamu kilichotokea jana. Jana Lema alijilipua kutokana na hali hiyo. Sasa suala lake naagiza liende kwenye kamati ya maadili kama ambayo Naibu  Spika alivyoagiza jana. Na suala lake liishe leo leo.

 “Ikiwezekana mambo yake kesho yawe yamekamilika, kwa hiyo kamati ya maadili saa nane kamili muanze kikao. Mheshimiwa Lema kuanzia saa saba uwe katika maeneo yale ili uweze kuthibitisha uliyosema jana. Na mimi niwaambie waheshimiwa wabunge, Spika Ndugai haogopi. Wanaofikiri sisi dhaifu, sio dhaifu. Nilishasema na kurudia.”

 Amesema, yeyote ambaye anataka kuingia kwenye anga zake, bunge lipo tayari kuwapeleka kwenye kamati.

 “Sisi tupo tayari na tutawapeleka huko kwenye kamati ile ambayo baadhi walisema ina udhaifu Fulani, basi Lema atakwenda huko  leo. Panapo majaaliwa tutaifahamu hatima yake na mwingine anayejiona yeye anaalikwa kwenye mkutano huo,” amesema Ndugai na kuongeza;

 “Yani tutanataka kuthibitisha Bunge hili la 11 lina uongozi na tutathibitisha kuwa hatumuogopi yeyote. Pia niwaambie  wananchi mambo mengine hawayaelewi vizuri, ipo misongo mingi ya mawazo humu ndani labda ndio inasababisha mambo hayo.” 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

Habari za SiasaTangulizi

Zanzibar watangaza rasmi kuwa shamba la Razaba ni mali yao

Spread the love  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imetangaza rasmi kwamba shamba...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi azindua Kamati ya Maridhiano Visiwani

Spread the love  RAIS wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Hussein...

error: Content is protected !!