May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Spika Ndugai amkaribisha Rais Samia bungeni

Job Ndugai

Spread the love

 

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amemkaribisha bungeni, Rais mpya wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. Anaripoti Mwandishi Wetu, Chato…(endelea).

Spika Ndugai amesema hayo leo Ijumaa tarehe 26 Machi 2021, mara baada ya kumalizika kwa misa takatifu ya kumwombea aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, Uwanja wa Magufuli uliopo Chato mkoani Geita.

Mara baada ya shughuli hiyo ya misa na salamu mbalimbali kutolewa, mwili wa Dk. Magufuli aliyefariki dunia tarehe 17 Machi 2021 katika hispitali ya Mzena, Dar es Salaam, utazikwa leo Ijumaa, nyumbani kwake.

Akitoa salamu za Bunge, Spika Ndugai amesema, walipokea kwa masikitika taarifa za kifo cha Dk. Magufuli ambaye aliwahi pia kuwa mbunge kwa miaka 20, kupitia jimbo la Chato.

Spika Ndugai amesema, Samia aliyeapishwa kuwa Rais, watampa ushirikiano wa kutosha ili aweze kuwatumikia vyema wananchi.

”Tunamkaribisha bungeni, pale ndipo ataweza kuongea na Watanzania wote. Tunakukaribisha kwa muda utakaoona wewe unafaa,” amesema Spika Ndugai

Naye Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amesema, utumishi wa Hayati Magufuli “ulikuwa wa kuhoji na kujitoa kwa wananchi.”

Profesa Juma amesema, mahakama ya Tanzania inatambua mchango mkubwa na hakuna eneo ambalo hakuligusa enzi za utawala wake.

Amesema, kuna program ya maboresho ya mahakama “na hadi miaka kumi ya utawala wake anaondoka, tulipanga kuboresha kabisa mahakama za mwanzo na kila mkoa uwe na mahakama kuu. Lakini haya tutayaendeleza.”

Profesa Juma amemhakikishia ushirikiano wa kutosha, Rais Samia Suluhu Hassan.

error: Content is protected !!