May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Spika Ndugai amjibu Mbowe

Job Ndugai Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania

Spread the love

HOTUBA ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ‘imemkera’ Spika wa Bunge, Job Ndugai. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Kwa kifupi akijibu kile kilichomo kwenye hotuba ya Mbowe aliyoitia Jumapili ya tarehe 11 Aprili 2021, Spika Ndugai amesema ‘Mbowe anapotosha umma.’

“…sasa huyo rafiki yangu Freeman Mbowe, alikuwa Ulaya huko, sasa katumwa na watu wake huko, anapotosha mambo,” amesema.

Kwenye hotuba yake, pamoja na mambo mengine Mbowe alilituhumu Bunge kwa vitendo vya rushwa.

Hivyo, Spika Ndugai ameagiza Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na ile ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), kufanya uchambuzi wa haraka Ripoti ya Mdhibiti na Mkuguzi wa Hesabu za Serikali (CAG).

Na kwamba, baada ya kufanya uchambuzi huo, uwasilishwe bungeni kwenye mkutano wa nne badala ya mkutano wa tano.

Spika Ndugai amesema, amefanya uamuzi huo kwa kuwa, ripoti hiyo imekuwa ikipotoshwa kwa kiwango kikubwa.

Kiongozi huyo wa bunge amesema, Watanzania wengi hawana uwelewa wa kuchambua taarifa za kihasibu. Kutokana na hivyo, kunaweza kusababisha upotofu.

error: Content is protected !!