June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Spika Makinda ahimiza 50/50

Anne Makinda, aliyekua Spika wa Bunge la Tanzania

Spread the love

SPIKA wa Bunge Anne Makinda amewahimiza wanawake kugombea nafasi za kisiasa  ili ipatikane asilimia 50/50 katika ili kuondoa mfumo dume. Anaandika Faki Sosi na Hamisi Mguta, DSJ … (endelea).

Hayo aliyasema Jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya wanawake Afrika yaliyoandaliwa na Shirika la Wanawake Katika Sheria na Maendeleo ya Afrika(WILDAF), yaliyofanyika leo Kilimanjaro Hoteli.

Wakati akizindua Ripoti inayohusu Hali ya Haki za Wanawake katika Nyanja mbalimbali za Maendeleo Spika Makinda amesema kuwa wanawake wamepiga hatua katika nyanja za kisiasa kwa asilimia 35 bungeni kwa kubakiza asilimia 15 kwa kuweka 50/50.

Amesema asilimia ya wanawake wameongezeka katika nyanja mbalimbali za serikali Mawaziri asilimia 32, Manaibu Mawaziri asilimia 21, Makatibu Wakuu asilimia 31, Wabunge asilimia 35, majaji asilimia 38 na sehemu nyingine za kisiasa.

Aidha, amesema kuwa wanawake waungane bila kujali itikadi za vyama vyao ili wazidi kuimarika katika Nyanja hiyo ya kisiasa na Nyanja nyengine za kiuchumi, kielimu na nyanja nyingine.

Naye Wakili Clarence kipobota ambaye aliyeandaa taarifa hiyo iliyobeba utafiti wa jinsia na haki za wanawake na watoto amesema kuwa Madawati mbalimbali ya sheria yamesaidia kuwepo kwa utorowaji wa taarifa ya unyanyasaji wa haki za wanawake na kupunguza kwa kasi unyanyasaji huo

Maadhimisho hayo yanayoazimishwa kila Mwaka tarehe 31 julai Afrika nzima yenye kauli mbiu ‘Uchaguzi 2015 Zingatia Usawa wa Kijinsia Kuleta Mabadiliko Chanya’.

error: Content is protected !!