Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Spika Job Ndugai ‘kutimuliwa,’ wabunge CCM wanoa makucha
Habari za Siasa

Spika Job Ndugai ‘kutimuliwa,’ wabunge CCM wanoa makucha

Job Ndugai
Spread the love

 

NAFASI ya Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kuendelea kukalia kiti hicho Bungeni iko shakani. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Duru za siasa kutoka na ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), zinadai kauli ya Ndugai kuhusu kubeza mikopo, imemdhalilisha Rais Samia Suluhu Hassan, nchi na wananchi wake, hivyo amepoteza sifa ya kuwa kiongozi wa mhimili huo wa dola.

Mbali na mashambulizi kutoka ndani ya chama chake cha CCM, Ndugai pia amekuwa akipokea mashambulizi kutoka vyama vya upinzani.

Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa zamani wa Iringa Mjini (Chadema), amesema Ndugai amemdhalilisha Rais Samia.

“Bila kumung’unya maneno, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa nchi, amedhalilishwa na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Spika Ndugai kwa kinachoitwa ukopaji utakaosababisha nchi kupigwa mnada. Tangu JPM (Rais John Pombe Magufuli) atutoke, mamlaka ya urais inajaribiwa,” amesema Mchungaji Msigwa.

Soma zaidi habari hii katika Gazeti la Raia Mwema la leo Ijumaa 31 Desemba 2021 kujua undani wa sakata hili.

2 Comments

  • Kiukweli Kila kiongozi anakuja namgumo wake wa kiongoza kwamfano Nyerere kaja na mfumo wake Mwinyi kaja na mfumo wake mkapa kaja na mfumo wake Kikwete kajana na mfumo wake Magufuri pia kaja na mfumo wake mama Samia pia alikadhalika kaja na mfumo wake kwahiyo tusi sisitukiwa kama wananchi tuwewapole tukubaliane na mfumouliopo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yaiangukia Serikali kunusuru wananchi Liwale, Nachingwea

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimeitaka Serikali kuchukua hatua za haraka...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari za Siasa

Gridi ya Taifa kufumuliwa kukabiliana na katizo la mgao wa umeme

Spread the love  WAZIRI wa Nishati, Januari Makamba, amesema Serikali ina mpango...

error: Content is protected !!