Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Spika ang’aka kukatika kwa umeme, atoa maagizo
Habari za Siasa

Spika ang’aka kukatika kwa umeme, atoa maagizo

Job Ndugai Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania
Spread the love

 

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai ameiagiza Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kukaa na wizara ya nishati ili kupata ufafanuzi unaoridhisha kuhusu mipango ya wizara hiyo katika kukabiliana na tatizo la kukatika kwa umeme nchini. Anaripoti Gabriel Mushi… (endelea).

Amesema kukatika kwa umeme limekuwa tatizo hivyo kamati hiyo iwaite wajumbe wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ili wajue uzito wa kazi waliyopewa vinginevyo tatizo ni kubwa.

Ndugai ametoa agizo hilo leo tarehe 2 Novemba, 2021 bungeni jijini Dodoma baada ya wabunge kumbana Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato kuhusu tatizo hilo ambalo limekuwa kero katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Wa kwanza alikuwa Mbunge wa Manyoni Magharibi, Yahaya Massare (CCM) ambaye amesema kila ifikapo siku za Jumamosi na Jumapili lazima umeme ukatike katika Halmashuri ya Itiji mkoani Singida.

Akijibu swali hilo, Naibu waziri huyo amesema kutokana na mabadiliko makubwa yaliyofanywa ndani ya wizara na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), anaamini wenzake waliopewa dhamana watakwenda kukidhi mahitaji ya Watanzania.

“Pia bajeti ya Tanesco imewekewa mechanism kuhakikisha inaziba mianya ya mapato kuvuja ili kuimarisha kukatika kwa umeme. Sababu zipo nyingi ila zilizo ndani ya uwezo wetu tunazifanyia kazi,” amesema.

Mbunge wa Kilombero, Abubakar Assenga (CCM) naye amesema katika Mji mdogo wa Ifakara kila ifikapo Jumanne na Alhamisi, umeme umekuwa ukitakatika huku miradi mingi ya umeme nayo ikisuasua.

Wakati Mbunge wa Sengerema, Hamis Tabasamu naye amesema umeme hukatika zaidi ya mara 10 kwa siku katika jimbo lake.

Akijibu maswali hayo ya nyongeza, Naibu Waziri huyo amesisitiza kuwa hakuna mgawo wa umeme kwa maeneo yote ya nchi kwa sasa kwani upo umeme unaotesheleza mahitaji ya nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!