July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Spika akerwa wabunge wanaotangatanga bungeni

Bunge la Tanzania

Spread the love

 

SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amewataka wabunge kuwa na staha wakiwa ndani ya Bunge na kuacha kutangatanga na kupiga kelele. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Spika Tulia ametoa onyo hilo leo tarehe 23 Mei, 2022 bungeni jijini Dodoma wakati akitoa muongozo kwa wabunge baada ya kipindi cha maswali na majibu.

Amesema wabunge wanatakiwa kuzingatia kanuni ya 73 ya Bunge inayozungumzia kuhusu staha ndani ya Bunge.

“Nimesimama hapa lakini naona kuna wabunge wanazungumza… inabidi usikilize kwa sababu huenda jambo linalosemwa hapa yanakuhusu wewe.

“Lingine nishawahi kusema huko nyuma, niseme tena leo, wageni wanaokuja hapa wengine wanakuja kwenye bajeti ya siku husika, wengine wanakuja hapa kututembelea na kujifunza shughuli za Bunge.

Dk. Tulia Ackson, Spika wa Bunge la Tanzania

“Kwa hiyo tufuate zile kanuni zetu za utaratibu humu ndani, ikiwa ni pamoja na kanuni 73 inayozungumzia kuhusu stahaha ndani ya Bunge,” amesema.

Amesema wapo wabunge siku nzima wanazunguka kiti kimoja kwenda kingine.

“Hata akiulizwa jambo gani limejadiliwa hiyo siku, hajamsikia mchangiaji hata mmoja. Kwa hiyo waheshimiwa wabunge kanuni zetu zimetaja wazi kutangatanga ndani ya bunge bila sababu.

“Tulizingatie hili kwa sababu kanuni yetu ndio inasema hivyo na imetumia maneno hayo si mimi ninayesema ndivyo ilivyosema, kutangatanga humu ndani hairuhusiwi,” amesema.

error: Content is protected !!