August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sopu aibuka kinara wa mabao ASFC

Spread the love

 

MABAO matatu aliyofunga kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Yanga, yamemfanya mshmabuliaji kinda wa Coastal Union, Abdul Seleman Sopu, kuibuka kuwa kinara wa upachikanaji mabao kwenye michuano hiyo Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo ulipigwa hii leo tarehe 2 Julai 2022, kwenye dimba la Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha na kushudia Yanga ikiibuka na ushindi kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-1, kufuatia kutoshana nguvu kwenye dakika 120 kwa mabao 3-3.

Mchezo huyo leo ameandika bao lake la tisa na Hat Trick yake ya pili kwenye michuano hiyo, huku moja akifunga kwenye michezo ya hatua ya awali dhidi ya Top Boys.

Mabao ya leo ya Coastal Union ambayo yaliwekwa kambani na mchezaji huyo, yalipachikwa kwenye dakia 120 za mchezo.

Mara baada ya mchezo huo kinda huyo wakati akifanya mahojiano alisema kuwa, walijiandaa kushinda mchezo wa leo lakini bahati ikawa upande wa Yanga.

“Kitu kilichotutoa mchezo ni jinsi Yanga walivyokuwa wanarudisha mabao, namdshukuru mungu kwa matokeo haya ya le.” Alisema Sopu

Akizungumza juu ya kuibuka kuwa kinara wa upachikaji mabao katika michuano hiyo, kinda huyo alisema kwamba toka msimu ulivyoaanza alijipanga kuwa mfungaji bora.

“Inanipa furaha kwasababu tangu mashindano yaanaza nilijipanga kuwa mfungaji bora namshukuru Mungu nimeweza kuwa mfungaji bora.” Alisema mchezaji huyo

error: Content is protected !!