June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sophia Simba awaponda wabunge CCM

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM, (UWT), Sophia Simba (kushoto) akiwa na Rais Jakaya Kikwete

Spread the love

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM, (UWT), Sophia Simba, amekiri wazi kwamba wabunge vijana kutoka vyama vya upinzani wanaweza kujenga hoja wawapo bungeni tofauti na wale wa Chama tawala (CCM). Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Mbali na hilo aliwataja wajumbe wa Baraza Kuu Maalum la umoja huo kuwachagua wabunge watakaozunguza bungeni kwa kujenga hoja badala ya kuwepo bungeni kama watalii.

Alitoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa baraza hilo mjini hapa , Simba amesema kuna maneno asiyoweza kuyaongea yeye bungeni lakini vijana wanaweza kuyazungumza kutokana na malezi.

Alisema kuna kila sababu ya kuwachagua viongozi ambao wataweza wana uwezo mkubwa wa kutetea hoja pindi wawapo bungeni badala ya kwenda huko kwa lengo la kutambishiana kwa mavazi.

“Chagueni watu watakaoengea bungeni. Nyie mmefundishwa kujiamini, kuna maneno ambayo mnaweza kuyasema lakini mimi siwezi kuyasema,”amesema.

Mbali na hilo Simba amesema uchaguzi wa mwaka huu ni tofauti na chaguzi zilizopita, wanawake watakaochaguliwa wahakikishe wanafanya kampeni kwa lengo la kukipatia ushindi chama chao.

“Kuna jambo baya ambalo linafanywa na baadhi ya wabunge wa Viti Maalum wakichaguliwa wanaenda zao Ulaya kununua nguo na mabegi jambo kubwa ni kutambiana na kuoneshana mavazi wawapo bungeni.

“Hawaonekani kwenye kampeni, safari hii tunawaangalia. Sio kupaka lipstic tu bali mje kufanya kampeni,”amesema.

Amesema katika uchaguzi mkuu uliopita walipata tabu kwasababu walipokuwa wakifika kwenye kampeni wilayani wabunge hao wa kuteuliwa walikuwa hawaonekani.

Simba amesema pia UWT iliwataka makada watakaoshinda ubunge wa Viti Maalum kutoa Sh100,000 kwa ajili ya kuchangia ununuzi wa magari ya umoja huo lakini waligoma kutoa.

Kabla ya kuanza kwa kwa kikao hicho baadhi ya wajumbe wa baraza hilo walihoji juu ya kutoonekana kwa majina yote ya wagombea Viti Malum kupitia Jumuiya ya wazazi.

Hata hivyo, Msimamizi wa Uchaguzi, Zakhia Meghji, aliwaondoa hofu kuwa majina yote ya walioshinda mkoani kupitia jumuiya hiyo yatapigiwa kura katika baraza hilo.

Kauli iliyoungwa mkono na Katibu Mkuu wa UWT, Amina Makilagi, aliyewaomba radhi wajumbe kuwa hawakuweza kuingiza maelezo binafsi ya wagombea viti maalum kupitia jumuiya ya wazazi na vijana kutokana na kuchelewa kuyapata majina hayo.

Akanusha kumfuta Lowassa

Simba amesema hana mpango wa kuhama CCM kama baadhi ya watu wanavyoandika katika mitandao ya jamii.

Simba ni miongoni mwa wajumbe wa Kamati Kuu (CC) waliojitokeza hadharani na kumtaka kuwa kanuni zilikiukwa katika zoezi la uchujaji wagombea.

Wengine waliojitokeza kupinga maamuzi ya CC hadharani ni Dk. Emanuel Nchimbi na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa.

Simba amesema   hajawahi kufikiria wala kupanga kuhama chama hicho.

“Nafahamu kwamba CCM ndiyo iliyowezesha watu kunifahamu, naringa, natamba kwa sababu ya CCM. Nimejipanga kuongoza timu ya wanawake kunamepeleka Dk. John Magufuli Ikulu, tumevunja kambi zetu zote tumebaki na kambi moja ya tingatinga,”alisema.

Kuhusu Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Simba amesema kila mtu anahama chama kwa sababu zake na kwamba yeye hana sababu ya msingi ya kufanya hivyo.

“Yeyote atakayeondoka CCM, hatupi mtikisiko ni uhuru wake kufanya hivyo, CCM haiwezi kutetereka kwa wachache wanaohama sisi mamilioni hatuhami na tupo strong (imara),” amesema Simba.

Mbwembwe za wapambe

Kabla ya kuanza kwa kikao cha baraza hilo, wapambe wa wagombea walionekana wakiwa wameshika mabango yanayowanadi wagombea wao wamnaowaunga mkono.

Wapambe hao wakiwa wameshikilia mabango walikuwa wamesambaa hadi nje ya lango kuu la kuingilia katika jengo la makao makuu ya chama hicho maarufu kama White House.

Miongoni mwa mabango yaliyoonekana katika eneo hilo ni la Rita Mlaki, Halima Bulembo na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angella Kairuki.

Uchaguzi wa wawakilishi wa wabunge wa viti maalum kutoka makundi mbalimbali ya Jumuiya za wazazi, vijana, wafanyakazi, watu wenye ulemavu na vyuo vikuu.

error: Content is protected !!