March 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Somalia yamtimua mjumbe wa Umoja wa Mataifa

Nicholas Haysom

Spread the love

SERIKALI ya Somalia imemfukuza Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa (U.N) nchini humo, Nicholas Haysom kwa sababu ya kuingilia mambo ya ndani ya taifa hilo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Somalia, Haysom anadaiwa kuingilia wazi wazi masuala yake ya ndani.

Wizara hiyo imeeleza kuwa, imetoa taarifa za kufukuzwa kwa mwakilishi huyo kwa Katibu Mkuu wa U.N, Antonio Guterres.

Hivi karibuni vyombo vya habari nchini Somalia, viliripoti kwamba Haysom aliitaka serikali kutoa maelezo kuhusu kushikiliwa kwa wafuasi 15 na kiongozi wa zamani wa kundi la kigaidi la Al-Shabab ambaye aliwahi kushriki kinyang’anyiro cha uchaguzi wa nchi hiyo, Mukhtar Robow.

Haysom aliteuliwa na Guterres kuwa mwakilishi wa U.N nchini Somalia mnamo mwezi Septemba mwaka 2018.

error: Content is protected !!