July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Somalia hali si shwari

Spread the love

HALI ya Somalia ni tete kutokana na tishio la njaa ambapo tayari Umoja wa Mataifa (UN) umetoa wito kwa mataifa mbalimbali kuelekeza misaada yeke kwenye nchi hiyo.

Umoja huo unaeleza kuwa, msaada huo wa chakula unaweza kusaidia zaidi ya watu milioni moja na laki moja ambao wanateseka kutokana na njaa nchini humo.

Kwa mujibu wa UN na mashirika ya kutoa msaada yameeleza kuwa msaada unaohitajika kutoka kwenye mataifa mbalimbali unakadiriwa kufikia kiwango cha Dola za Marekani milioni 885.

Zaidi ya watu milioni tano wanaendelea kuteseka na njaa kutokana na kwamba, wito umetolewa kwa mataifa hayo kutoa misaada ya chakula nchini Somalia.

Taarifa ya UN inaeleza kuwa zaidi ya watoto 310,000 ni miongoni mwa wanaoathirika na njaa nchini gumo huku wakikabiliwa na tishio kubwa la kuangamia kutokana na baa la njaa na utapia mlo endapo mataifa mbalimbali hayatajitokeza kutoa misaada hiyo.

Hata hivyo, taarifa zaidi zinaeleza kuwa shughuli za kusambaza misaada zimeathirika kwa kubwa kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha, usalama na mvua ya el nino inayoendelea kunyesha kwenye sehemu kadhaa.

Peter De Clrecq ambaye ni Mratibu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya misaada ya kibinadamu nchini Somalia amesema, wito huo ni muhimu na utasaidi watu hao waliokimbia vita nchini Somalia hasa katika maeneo ya Baido, Bossaso, Gaalkayo, Kiismayo na Mji Mkuu wa nchi hiyo, Mogadishu.

error: Content is protected !!