October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Solskjaer ampigia chapuo Greenwood England

Spread the love

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amempigia debe kinda wake, Mason Greewood katika kikosi cha timu ya Taifa ya England, kutokana na kiwango alichokionyesha kwa hivi karibuni. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Greenwood ambaye mwenye umri wa miaka 18, hivi karibuni amekuwa na kiwango kizuri kwa kufanikiwa kufunga mabao matatu kwenye michezo dhidi ya Bournemouth na Brighton yote ya Ligi Kuu nchini England.

Kocha huyu amesema kuwa kama mchezaji huyo anaweza kumudu kucheza ndani ya Manchester United basi pia ataweza kucheza kwenye klabu na timu yoyote kwa sababu ana ubora ambao wengine hawana.

“Anaweza kucheza kwenye timu ya wakubwa England au hata chini ya miaka 21, mimi sitajali, najua anafanya vizuri kwetu na jambo kubwa kuwa naye,” alisema kocha huyo.

“Kama ameweza kumudu kucheza Manchester United kwa hiyo anaweza kumudu kucheza timu yoyote na Mason anaubora ambao wengine hawana,” aliongezea Solskjaer.

Greenwood ambaye amelelewa kwenye kituo cha Manchester United mpaka sasa ameshacheza michezo 29 ya Ligi Kuu England, na kufunga jumla ya mabao nane toka alipopandishwa kwenye timu ya wakubwa.

error: Content is protected !!