July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Soko Mawasiliano kufunguliwa Julai

Kituo cha daladala Mawasiliano

Spread the love

MENEJA wa Vituo vya Mabasi katika maeneo ya Mawasiliano, Makumbusho na Tegeta, Elichilia Hamis amesema, Soko Kuu la Mawasiliano linatarajiwa kuanza kutumika mwishoni mwa Julai mwaka huu. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Akizungumza na mwandishi wa gazeti hili Hamis amesema, soko hilo lina uwezo wa kubeba wafanyabiashara 312 kutoka sehemu tofauti Jijini Dar es Salaam.

Hamis amesema, amepokea barua mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara wakiomba nafasi katika soko hilo na kwamba;

“Wafanyabiashara wanaotaka kupata sehemu ndani ya soko hili wanatakiwa kupeleka barua kwa viongozi wao wa kata ambapo kila kata wanachukuliwa wafanyabiashara sita na baadaye hupelekwa kwa Mkurugenzi wa Jiji kisha kufikishwa kwangu kwa ajili ya kusajiliwa,” amesema Hamis.

Hata hivyo Hamis amesema, licha ya kuwepo kwa tuhuma nyingi kuhusu ucheleweshaji wa ujenzi huo, manispaa haihusiki.

“Manispaa haihusiki na kuchelewesha ujenzi bali ni kampuni iliyopewa kazi hiyo imeshindwa kwenda na muda kutokana na sababu mbalimbali,” amasema.

Mkandalasi wa soko hilo, Ibrahim Sadiki amegoma kuzungumzia sababu za kuchelewa kwa ujenzi huo.

 “Siwezi kuzungumzia kuhusu tatizo la kutomaliza kazi kwa muda tuliopangiwa kwani kuna kiongozi wangu ambaye ndio mmliki wa Kampuni ya Delmonte (T) LTD.”

Licha ya juhudi za kumtafuta Mkurugenzi wa Kampuni hiyo kutofanikiwa, Sadiki ameendelea kusisitiza kuwa, “hadi kufikia Julai mwishoni tutakuwa tumemaliza maana palipobaki ni padogo ambapo ni kumalizia choo tu kisha tukabidhi.”

Mbali na kutokamilika kwa ujenzi wa soko hilo kwa wakati, bado kumekuwa na tatizo kubwa la ubovu wa barabara iendayo katika Kituo cha Mabasi cha Mwasiliano ambapo madereva na watumaji wengine wa barabara hiyo wamekuwa wakilalamikia kwa muda mrefu bila majibu.

Hamis akifafanua hilo amesema, pesa za ujenzi wa barabara hizo zipo tayari na kwamba, kinachokwamisha ujenzi huo ni malipo kwa watu waliobomolewa nyumba zao wakati wa kutanua barabara.

“Plani yetu ilikuwa ni kupata barabara pana ndipo ikapelekea kwa baadhi ya nyumba kubomolewa ambapo inabidi walipwe ndipo ujenzi uendelee.”

Anesema, Halmashauri ilitarajia kuanza ujenzi huo Agosti mwaka huu “kilichotukwamisha ni hao waliojitolea kutoa msaada kwa kuwalipa waathirika lakini bado tunaendelea kuboresha baadhi ya vitu ili kuboresha mazingira.”

error: Content is protected !!