
Spread the love
MABANDA takribani 1,000 ya wafanyabiashara katika Soko la Mlango Mmoja lililoko jijini Mwanza yameteketea kwa moto alfajiri ya leo tarehe 28 Septemba 2018. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Taarifa ya tukio hilo imethibitishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Jonathan Shana.
Kamanda Shana ameeleza kuwa, kikosi cha uokoaji kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kinaendelea na jitihada za kuudhibiti moto huo ambapo zoezi hilo linaendelea vizuri.
Aidha, Kamanda Shana amesema chanzo cha moto huo hakijajulikana licha ya baadhi ya mashuhuda katika tukio hilo wakidai kuwa umesababishwa na baadhi ya mama lishe walioacha majiko yao yakiwa na moto.
More Stories
Wanafunzi walilia madarasa Mtwara, Silinde awajibu
LSF, NGO’s zajadili mfumo upatikanaji haki Tanzania
Majaliwa atoa maagizo kwa wazazi, walezi