January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Soko la Dunia kuchangia kushuka kwa bei ya mafuta

Spread the love

MAMLAKA ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia kutaendelea kushusha bei ya mafuta nchini. Anaandika  Eunice Laurian…(endelea)

Katika taarifa yake kwa umma, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi alisema, licha ya kushuka kwa bei hizo za mafuta katika soko la dunia, hazitakuwa zikishuka kwa wakati huo huo hapa nchini.

“Kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia kutaendelea kushusha bei hapa nchini japo si kwa wakati huo,”Ngamlagosi alisema.

Aliongeza kuwa kumekuwa na upotoshaji kwamba Ewura haishushi bei za mafuta kwa kuwa kushuka kwake kutaathiri mapato yake, lakini ukweli ni kwamba tozo ya Mamlaka hii inatokana na lita za mafuta na si bei.

“Iwapo Ewura ingetaka mapato mengi, basi ingeongeza wingi wa lita za mafuta yanayoingia hapa nchini, na si kutegemea kupanda kwa bei. Hivyo basi kushuka au kupanda kwa bei hakuna uhusiano wowote na ongezeko la tozo kwa Ewura,”alieleza.

Alisema, Mamlaka hiyo itaendelea kutimiza wajibu wake kisheria katika sekta ndogo ya mafuta hapa nchini, ikiwemo upangaji bei kikomo za mafuta na kuzisimamia katika maeneo yote nchini.

Mkurugenzi huyo alisema kwa mwaka huu, bei ya petroli ilishuka toka kiwango cha juu zaidi, Septemba 2014, Sh 2,267 kufikia Sh 1,898 kwa lita ikiwa ni kupunguka kwa Sh 369 kwa lita. Bei ya dizeli ilishuka toka kiwango cha juu zaidi, Aprili 2014, ilipokuwa ikiuzwa Sh 2,149 na kufikia Sh 1,747 kwa lita Januari 2016, hii ikiwa ni kupungua kwa Sh 402 kwa lita.

 

error: Content is protected !!