July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Snura, ‘Chura’ wapigwa kitanzi

Spread the love
WIMBO na Chura na video yake vimepigwa marufuku kuoneshwa ama kupigwa kwenye maonesho yote ya hadhara ya mwanamuziki wa kizazi kipya, anaandika Regina Mkonde.
Pia shughuli za Snura Mushi, msanii na mtunzi wa wimbo huo zimesimamishwa mpaka atakapokuwa tayari kufuata taratibu zilizotolewa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kikao kilichofanywa jana na Wizara ya Habari, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) na kwamba, kikao hicho kilibaini kuwa, video ya wimbo huo haikuwa na maadili pamoja na msanii huyo kufanya kazi bila kibali kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (Basata).
Akizungumza na waandishi wa habari leo Zawadi Msala, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Ofisi ya Wizara ya Habari jijini Dar es Salaam amesema, video ya wimbo wa Chura imsetishwa hadi itakapofanyiwa marekebisho.
“Usitishwaji huo umetokana na maudhui ya utengenezaji wa video hiyo ambayo haiendani na maadili ya Mtanzania, na kwamba wizara imesitisha wimbo wa Chura hadi itakapofanyiwa marekebisho,” amesema Msala.
Amesema, Snura hatoruhusiwa kufanya maonesho ya hadhara hadi atakapokamilisha taratibu za usajili wa kazi za sanaa katika Ofisi za Basata.
“Serikali imechukizwa na kazi hiyo ambayo situ inadhalilisha tasnia ya muziki bali inadhalilisha utu wa mwanamke na inaifanya jamii kuanza kuhoji hadhi ya msani, weledi na taaluma ya sanaa kwa ujumla,” amesema.
Patrick Kipangula, Mwanasheria wa Wizara ya Habari amesema, Snura amevunja sheria ya filamu na michezo ya kuigiza ya mwaka 1976 kifungvu Na. 3 Kanuni ya 24.
“Kuendesha kazi bila ya kuzingatia sheria ni kosa, Snura hajajisajiri, ametoa kazi bila ya kupata kibali pamoja na kuitoa nyimbo bilka ya kuipeleka sehemu husika kwa aajili ya kuifanyia ukaguzi ili kuithibitisha kama inafaa,” amesema.
Aidha, Wizara imemtaka Snura kuiondoa video ya wimbo wake katika mitandao ya kijamii na kuvitaka vyombo vya habari kutoicheza wimbo huo.
“TCRA inafuatilia agizo la wizara juu ya kuondolewa na kutosikilizwa kwa wimbo  huo na kwamba mtu yeyote akibainika anarusha wimbo huu kwa watu wengine atachukuliwa hatua kali za kisheria,” amesema Msalla.
Msalla amesema kuwa, kusitishwa kwa wimbo wa Snura kutasaidia kuikanya jamii hususani wasanii kutokana na kwamba hawatathubutu kutoa nyimbo pasipo kujiridhisha kama ina maudhui chanya kwa jamii.
error: Content is protected !!