August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Snura awaomba radhi Watanzania kwa video ya Chura

Spread the love

BAADA ya wimbo wake wa Chura kufungiwa na Serikali jana, Msanii Snura Mushi, leo ameibuka na kuomba radhi na kuahidi kutekeleza maagizo ya serikali, anaandika Regina Mkonde.

Wimbo huo ulipigwa marufuku na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo kwa kuiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuufungia wimbo huyo kutokana na kutoendana na maadili ya Mtanzania.

Mamlaka hiyo ilisema kazi hiyo inadhalilisha tasnia ya muziki. Serikali ilipiga marufuku maonyesho yote ya hadhara ya Snura hadi pale atakapokamilisha usajili wa kazi zake za Sanaa katika Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).

Snura amesema anawaomba radhi Watanzania wote kwa kilichotokea na tayari amechukua hatua na kusajiliwa rasmi kwa ajili ya shughuli za kisanii.

error: Content is protected !!