Tuesday , 18 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Skendo za kuhamia CCM, Kubenea afura, ashambulia Mwananchi
Habari za SiasaTangulizi

Skendo za kuhamia CCM, Kubenea afura, ashambulia Mwananchi

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo
Spread the love

Taarifa kwa umma

NIMEONA picha yangu kwenye gazeti la leo Jumanne la MWANANCHI likinihusisha mimi na kutaka kuhama chama changu na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Napenda kueleza masikitiko yangu kuona gazeti lililokuwa linaheshimika katika jamii, linajiingiza katika kuandika habari ambazo chanzo chake ni mitandao ya kijamii ya WhatsApp na Jamii Forum na zinazosambazwa na watu wenye nia ovu dhidi yangu.

Narejea tena na tena, kwamba sina mpango wa kuondoka Chadema. Sijawahi kuzungumza na mtu yoyote yule wa CCM kuwa nataka kujiunga na chama chao.

Hii ni kwa sababu, mpaka sasa, mimi binafsi, sijaona sababu zinazojitosheleza kunishawishi kuondoka Chadema na kujiunga na chama kingine.

Ninafahamu wazi kuwa wapo watu ndani ya Chadema wanaotaka nikihame chama changu, ili kukidhi maslahi yao binafsi.

Napenda kuwahakikishia kuwa siondoki na hakuna wa kuniondoa.

Wanaodhani kuwa mimi kuwamo kwangu huku ni kero kwao, basi nawaomba waondoke wao.

Watuachie sisi chama tutakaosalia. Tunaahidi tutakijenga, kikiimarisha na kukiendeleza hadi kuelekea kushika dola.

Nitaendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa Chadena na nitaendelea kuwatumikia wananchi wangu wa Ubungo, hadi nimalize kipindi changu cha Ubunge.

Kuhusu gazeti la MWANANCHI, naomba kulishauri mambo mawili makuu:

Liache kuandika habari za kuokoteza juu yangu zinazohusu madai ya kuhama chama.

Litumie muda huu, kufanya uchunguzi yakinifu wa wapi alikofichwa; na au nani waliomteka na kumshikilia mwandishi  wao wa habari mahiri za uchunguzi aliyetoweka takribani miezi mitano iliyopita, huko Kibiti, mkoani Pwani.

Hiyo ndio kazi ya kitume ambayo gazeti kama MWANANCHI linapaswa kuifanya.

Saed Kubenea,

Mbunge wa Ubungo.

IMG-20181009-WA0020

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Mazingira magumu ya JPM yamechangia ‘Comedy Journalism’

Spread the loveMwenyekiti wa Kamati ya kufuatilia hali ya uchumi wa vyombo...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

RC Chalamila: Nimeacha ubabe

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chamalila amemthibishia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia atoa ujumbe mzito Sikukuu Eid Al Adha

Spread the loveKATIKA kusherehekea Sikukuu ya Eid Al Adha, Rais wa Tanzania,...

BiasharaHabari za Siasa

Dk. Biteko aipongeza NMB kwa kuanzisha utoaji wa bima ya mifugo

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!